Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WAZIRI wa Maliasili na Utalii,Angellah Kairuki aliomba bunge kupitisha shilingi bilioni 348 bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kairuki ameliomba Bunge jijini hapa leo,Mei 31,2024 wakati akiwasilisha bajeti yake yenye viapaumbele nane huku akifafanua Kati ya fedha hizo,
Shilingi 250,884,083,000 zitagharamia Matumizi ya Kawaida na Shilingi 97,241,336,000 ni kwa ajili
ya Miradi ya Maendeleo.
“Fedha za Matumizi ya kawaida zinajumuisha Mishahara Shilingi
125,366,391,000 na Matumizi Mengineyo Shilingi 125,517,692,000.
“Fedha za Miradi ya Maendeleo
zinajumuisha Shilingi 18,074,661,000 fedha za ndani na Shilingi 79,166,675,000 fedha za nje,”amefafanua.
Na kuongeza”Fedha za Matumizi ya
Kawaida Shilingi 250,884,083,000 zinajumuisha Shilingi 30,695,909,972 kwa ajili ya Wizara na Shilingi 220,188,173,028 kwa ajili ya taasisi zilizo chini ya Wizara.
Amesema Kati ya fedha za Wizara, Shilingi 8,463,022,058 ni Mishahara na Shilingi
22,232,887,914 ni Matumizi Mengineyo. Fedha za taasisi zinajumuisha Shilingi 116,903,368,942 za Mishahara na Shilingi 103,284,804,086 za Matumizi Mengineyo.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato