Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Kiteto
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim, amempongeza Mbunge wa jimbo Kiteto Mkoani Manyara Edward Ole Lekaita kwa kushiriki Kikamilifu kwenye shughuli ya Kitaifa za kuupokea na kukimbiza mwenge wa uhuru ulipokua Wilayani Kiteto hadi kukabidhiwa kwake katika Wilaya ya Simanjiro.
Kaimu amesema hayo Jana wakati alipokua akiagana na wananchi na viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuingia Wilaya ya Simanjiro ambapo amesema kitendo cha Mbunge Lekaita kushiriki shughuli ya Kitaifa sio tu kuuenzi Mwenge wa uhuru bali ni kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere.
“Mheshimiwa Mbunge Ole Lekaita nakupongeza sana kwa kushiriki ipasavyo kwenye mbio za mwenge kwa mwaka huu wewe ni mzalendo mtu bingwa kabisa kwani umeonyesha ushirikiano mkubwa na viongozi wenzake wa Kiteto,” amesema Kaim.
Aidha Kaim amesema huo ni uzalendo mkubwa aliouonyesha Mbunge wa jimbo la Kiteto, ambapo amesema kuwa mwenge sio wa wananchi peke yao, bali ni wa pamoja na wananchi vya vyama vyote pamoja na viongozi wote wa vyama na Serikali.
MBUNGE wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara, Mh. Edward Ole Lekaita amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha nyingi na huku zikifanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo Jimboni humo.
Ole Lekaita ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mbio za mwenge wa uhuru Wilayani Kiteto mara baada ya kupata nafasi ya kuwasalimia wananchi wa Jimbo la Kiteto wakati wa kukagua, kuzindua, kutembelea na kuweka jiwe la msingi kwenye miradi ya maendeleo mbalimbali yenye thamani ya shilingi bilioni 2.4.
Miradi iliyotembelewa na mwenge wa uhuru mwaka 2023 Kiteto ni pamoja na kufungua madarasa mawili na ofisi ya shule ya msingi Esukuta na daraja Orkine.
Mwenge ulifungua shule mpya ya msingi Azimio na kupanda miti 500 na kuzindua na utunzaji wa mazingira shule ya sekondari NASA Matui na kuzindua klabu ya wapinga rushwa.
Pia, mwenge wa uhuru uliweka jiwe la msingi ujenzi wa majengo matatu hospital ya wilaya ya Kiteto na kuzindua mradi wa maji wa RUWASA Majengo mapya Kata ya Kaloleni.
Ole Lekaita amesema kupitia miradi mbalimbali iliyotembelewa na mwenge Kiteto na mingine iliyopo Kiteto ambayo haijapitiwa na mwenge, wamepiga hatua kubwa ya maendeleo hivyo wanamshukuru Rais Dkt Samia.
“Kwa niaba ya watu wa Jimbo la Kiteto nampongeza Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za maendeleo zilizofanikisha miradi ya sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu na mengine,” amesema Ole Lekaita.
Hata hivyo, amesema wakazi wa Kiteto hawana cha kumlipa Rais Samia ila wanamuombea afya njema, uzima na wanasubiri ifikapo mwaka 2025 kura zake zote za ndiyo wanazo wamezifichwa kwenye rubega.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi