Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala FANTA BONIFACE KAIJAGE amechangisha shilingi milioni. 1.2 katika harambee ya UWT Tawi la Mji Mpya kata ya Kipawa wilayani Ilala kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake wa UWT wafungue mradi wa kukodisha viti na maturubahi sehemu ya mtaji wa Tawi hilo.
Harambee hiyo ilifanyika katika Mkutano mkuu maalum wa Umoja wanawake Mji mpya ambapo Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT wilaya ya Ilala FANTA BONIFACE KAIJAGE alikuwa mgeni rasmi na Mgeni maalum Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka.
Akiendesha harambee hiyo ya mradi wa Viti vya UWT na Maturubahi ya UWT mji mpya mgeni rasmi FANTA KAIJAGE alichangia shilingi 300,000,Diwani Viti Maalum Cheka shilingi 100,000,Diwani Julieth Banigwa shilingi 100,000,GRACE ZOA ZOA sh,100,000,Mama Mazongera sh,100,000,Mwati Kasangara sh,100,000 Pendo Samwel sh;120,000 Alex Katembo sh,100,000 na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mji mpya Kipawa 150,000 .
Mjumbe wa UWT Wilaya Fanta aliwataka UWT Mji mpya pesa hiyo kutumia katika mradi wa Jumuiya ya wanawake ili kujikwamua kiuchumi waache kuwa tegemezi kwani watakapokuwa na mradi wa kuwawezesha kiuchumi watasimamia majukumu yao vizuri katika kujenga chama na jumuiya kua kuakikisha CCM ina shika dola katika chaguzi zake zote ikiwemo Uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
“Nawaomba wanawake wenzangu mchape kazi katika kushirikiana kujenga chama na Jumuiya yetu ili tuweze kumsaidia Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na kuakikisha wanawake wote wanampigia kura Rais Mwaka 2025 “alisema KAIJAGE.
Aidha aliwataka UWT kujenga umoja na mshikamano kwa maslahi ya chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake.
Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magreth Cheka aliwataka wanawake wa UWT kujenga umoja na mshikamano katika kutafuta fursa mbali mbali za kiuchumi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kukuza mitaji yao.
Magreth Cheka alizungumzia Mto Msimbazi kwa wananchi wa kipawa aliwapa pole wananchi wa eneo hilo mji mpya poleni mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ameshatatua kero hiyo kwa kuwapigiania Serikali Kuu hivi karibuni mradi huo utaanza rasmi kujengwa na kwa kuwekwa kingo na mradi wa DMDP kuondoa adha ya mafuriko.
Katibu wa umoja wanawake UWT tawi la Mji mpya ANNA MUSHI katika risala yake awali aliomba kwa mgeni rasmi FANTA BONIFACE KAIJAGE awawezeshe mtaji wa viti na maturubahi wawe wanakodisha iwe sehemu ya mtaji wa tawi hilo iwaongeze mapato.
Anna Mushi alisema kwa sasa 250 wote wanachama hai wa UWT viongozi wa tawi 14 Tawi la Mji Mpya ni miongoni mwa matawi kumi ya kata ya Kipawa ,ambapo upande wa Utawala lina matawi ya shina 13 Mtaa wa Karakata
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu