Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
KADA wa chama cha Mapinduzi CCM Selemani Kaniki, amewataka vijana wa Bodaboda mkoa Songea na Njombe kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan,na kufanya kazi za halali za kuwaingizia kipato wasifanye biashara halamu .
Kada Selemani Kaniki, alisema hayo katika vijiji vya Njombe na Songea katika vijiwe vya Bodaboda wakati wakuwapatia majaketi ya kujikinga na baridi wakati wa kufanya shughuli zao za kuwaingizia kipato.
“Vijana wangu wa Bodaboda kazi yenu mnayofanya ni nzuri msimamie taratibu za nchi na kufanya kazi za halali muweze kupata kipato cha kuweza kupata pesa ya kusomesha watoto wenu pia mumsaidie Dkt.Samia Suluhu Hassan msijiingize kujihushishe na Biashara nyingine ambazo si taratibu za nchi yetu “alisema Kaniki
Katika hatua nyingine aliwataka vijana wa Bodaboda kuwa makini na kufuata sheria za Usalama Barabarani ili kujiepusha kupata ulemavu na vifo
.
Alisema vijana wa Bodaboda wana jukumu kubwa la kuisaidia Serikali kujenga nchi pia ni walinzi wazuri wakifuata taratibu za nchi yetu hawawezi kufanya biashara halamu.
More Stories
Serikali yahimiza wananchi kutembelea vivutio vya utalii
Magunia ya kufungia tumbaku yakamatwa
Madereva 16,Mwanza wafungiwa leseni ya udereva