December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kada Kaniki achangia Mil. 1 CCM Majohe

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

KADA wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Selemani Kaniki, ametoa ahadi ya kuchangia shilingi milioni 1 kwa ajili ofisi ya chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Majohe.

Selemani Kaniki ,alitoa ahadi hiyo ya kuchangia pesa hizo kwa njia ya simu wakati Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde alipokuwa akiendesha Harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi VIWEGE B kata ya Majohe wilayani Ilala.

“Mwenyekiti wa ccm wilaya Said Sidde tunakuunga mkono Juhudi zako za kujenga chama cha Mapinduzi CCM ndani ya wilaya Ilala mimi Hassan Kaniki mdau wa michezo naunga mkono juhudi zako katika Harambee ya Tawi la ccm VIWEGE B nitachangia shilingi milioni 1 “alisema Kaniki kwa njia ya simu.

Katika Harambee hiyo Wana CCM wengine waliochangia Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi amechangia shilingi 500,000 Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala shilingi 500,000 ,Mjumbe wa Kamati ya Fedha Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Kelvin Wiliam 500,000 ,MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya tawi Upanga MASHARIKI Shellina Sodawala shilingi 500,000 Diwani wa Kata ya Majohe Paschal Linyamala Shilingi 150,000 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Viwege Amina Kapundi shilingi 150,000

Jengo la Chama cha Mapinduzi CCM Tawi la Viwege B kata ya ili liweze kukamilika linaitaji shilingi milioni 9 kumaliza ujenzi wake ambapo jengo hilo limejengwa na wana ccm wa Viwege wilaya ya Ilala.

Akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde amewataka wana ccm ndani ya wilaya Ilala wote kuiga mtaa wa viwege kujenga na wao ofisi za matawi ya chama cha Mapinduzi kwa ajili ya kukipa heshima chama chetu cha Mapinduzi katika harambee hiyo ilipatikana kash shilingi 1.5

Aidha Mwenyekiti Said Sidde Alimpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa viwege Amina Kapundi kwa kutekeleza Ilani vizuri ya chama na kuwa na mahusiano mazuri ndani ya chama na nje ya chama.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Viwege Kata ya Majohe wilayani Ilala Amina Kapundi aliwapongeza wadau wote waliochangia ujenzi wa ofisi ya CCM tawi sasa ujenzi wake unaenda kukamilika na Mbunge wetu wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa amesema atachangia .

Mwenyekiti Amina Kapundi alisema dhumuni chama cha Mapinduzi CCM tuondokane katika nyumba za Kupanga ili tuwe na Ofisi za chama zetu .

“Chama Cha Mapunduzi CCM viwege B Majohe tumemuhesimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ccm Viwege sasa tuna ofisi zetu na tunaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita kwa utekelezaji wa Ilani .