Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
KADA wa chama cha Mapinduzi Selemani Kaniki, ameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan , katika kusaidia sekta ya michezo na kukuza timu za REDE .
Kada Selemani Kaniki, alisema hayo katika ufunguzi wa mashindano ya REDE Chanika Jimbo la Ukonga alipokuwa akitoa jezi kwa timu ya Kimwani ambapo ameunganisha vijana katika michezo hiyo.
“Naungana na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta ya michezo kwa kuinua timu za vijana ziweze kufanya vizuri na timu za REDE zitambulike katika michezo yao kwani ni mchezo unaopendwa na wengi ” alisema Kaniki.
Kada Selemani Kaniki aliomba viongozi wengine wajitolee sana katika michezo hiyo kwani michezo ni afya pia ujenga udugu.
Selemani Kaniki alisisitiza vijana upimaji afya na kuepuka ufanyaji mambo maovu katika jamii sababu vijana ndio nguvu kazi ya Taifa la kesho.
Katika hatua nyingine Selemani Kaniki alimpongeza Mbunge wa jimbo la Ukonga Jery Silaa kwa juhudi anazo fanya kumsaidia Rais utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kwa usimamizi mzuri kuwekeza sekta ya Elimu na sekta ya afya katika jimbo la Ukonga ujenzi wa shule nyingi na vituo vya afya vya Serikali.
Wakati huo huo alimpongeza Diwani wa Kata ya Zingiziwa Maige Maganga kwa kubuni mashindano hayo ya Rede ili kuwaunganisha makundi ya Vijana .
Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde kwa kujitoa kwake katika ziara za kutatua kero na ziara za kuangalia utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM na kuwataka viongozi wengine wa chama kuiga mfano huo
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba