Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
JESHI la Wananchi wa Tanzania( JWTZ) linatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuasisiwa kwake na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwaka 1964.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3 ,2024, Kaimu Mkurugenzi wa habari na uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania( JWTZ) ambaye pia ni Msemaji wa Jeshi hilo Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema kwamba maadhimisho hayo yatafikia kilele chake Septemba Mosi mwaka huu kwa kufanyika kwa gwaride maalumu pamoja na kuonyesha silaha za kivita kuanzia JWTZ ilivyoanza na ilipo hivi sasa katika kuimarisha ulinzi wa Mipaka ya Tanzania.
Luteni Kanali Ilonda amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na shughuli mbalimbali za kijamii kama vile utoaji wa matibabu kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani kwa wananchi kwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano na Jeshi hilo tangu kuanzishwa kwake.
“Hospitali zote za Kanda za Kijeshi ikiwemo Arusha,Mwanza,Mbeya,Tabora,Zanzibar,zitatoa matibabu bure kwa wananchi ikiwemo magonjwa ya kuambukiza kama vile UKIMWI, na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile Shinikizo la Juu la Damu,Saratani ya Matiti,Tezi dume,Sukari, Maabara na Damu salama pamoja na magonjwa ya dhalura,hivyo nawaomba wananchi kujitokeza kupata huduma hii” amesema Luteni Kanali Ilonda.
Luteni Kanali Ilonda amesema kuwa katika maadhimisho hayo kutakua na mazoezi mbalimbali ya kivita yatakayofanyika katika Mikoa ya Dar es salaam,Pwani,Tanga na Morogoro hivyo amewaomba wananchi wasiwe na hofu pindi watakapoona zana za kivita ikiwemo vifaru na ndege vita zikipita katika makazi yao.
” Naomba niwatoe hofu wananchi wanapoona zana za kivita zinapita kwenye maeneo ya makazi yao wasiwe na hofu waendelee na shughuli zao za kiuchumi kama kawaida kwani zana hizo zinatumika tu katika zoezi la maadhimisho ya miaka stini ya Jeshi lao,ambapo mwaka huu tunataka maadhimisho haya yawe ya aina yake tofauti na maiaka mingine.
Aidha Luteni Kanali Ilonda amesema katika maadhimisho hayo Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) litashirikiana na Jeshi la Ukombozi wa Watu wa china kufanya zoezi la pamoja kuanzia Julai 29 hadi Agost 11,2024 katika maeneo ya Dar es salaam na Pwani ambapo vikosi vitakavyohusika katika zoezi hilo ni pamoja na Kamandi ya Maji,Kamandi Nchi kavu, Kamandi ya Anga, nakwamba zana zitakazotumika katika zoezi hilo ni pamoja na Meli vita na Ndege.
” Zoezi hili la Serikali kupitia JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China litakua ni kuwakumbuka waasisi wa majeshi haya akiweo Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa China wa awamu hiyo,lakini pia ni kumbukumbu ya miaka sitini ya JWTZ tangu kuanzishwa kwake,na pia ni kumbukumbu ya miaka sitini ya udugu na uhusiano wa mataifa haya mawili” amebainisha Luteni Kanali Ilonda.
Nakuongeza kuwa” Zoezi hili litafanyika Baharini na Nchi kavu hivyo litafanyika kwa uwazi ili wananchi wapate fursa yakujionea kupitia vyombo vya habari kwa wale ambao hawapo maeneo ya Baharini,lakini wale ambao wapo karibu na maeneo ya Baharini itakua fursa kwao kuona mbashala na itakua sehemu ya utalii kwao.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ