Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kimanga wamekuwa Mabalozi wa shule ya Msingi Kimanga Darajani kwa kuchangia Matofali ya UJENZI wa matundu kumi ya vyoo vya Shule hiyo.
Katika wiki ya MAADHIMISHO ya miaka 46 ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi CCM Jumuiya hiyo ya wazazi Kimanga lhughuli za kijamii zikiwemo Usafi kutembelea vituo vya afya na vituo vya watoto yatima .
Alisema Nyumba ni choo na shule ni choo shule inapokosa vyoo Mazingira yanakuwa si salama kwa Wanafunzi .
“Jumuiya yetu ya wazazi Kimanga tutakuwa Mabalozi wa shule hii Kimanga Darajani ina changamoto mbalimbali vyoo vichahe pamoja na Shule kukosa uzio hali inayopelekea Wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa tabu watu wanakatisha Eneo hilo la shule ” alisema Zayana .
Alisema yeye na Jumuiya yake ya Wazazi Kimanga watajenga matundu Kumi ya shule hiyo kutatua kero ya matundu ya vyoo .Mwenyekiti Zayana ametoa wito wazazi kuwa karibu na kamati za shule hiyo Ili kutatua kero na kukuza taaluma kwa Wanafunzi .
Wakati huo huo Mwenyekiti Zayana alipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta pochi la Mama kata ya Kimanga katika sekta ya Elimu kujenga madarasa Shule ya Msingi na Sekondari .
Katibu wa CCM Kimanga Salima Kinyogoli alitoa pongezi kwa Jumuiya ya Wazazi Kimanga kujenga mahusiano ya chama na Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi .
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Kimanga Darajani Stanley Chababa ameitaka Jumuiya nyingine kuiga mfano wa Jumuiya ya wazazi kwa kufanya jambo kubwa katika sekta ya Elimu .
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kimanga Darajani Heavenligh Naiso alisema shule ya Kimanga darajani imeanza mwaka 2010 kwa Sasa ina Wanafunzi 480 katika miaka Saba Maendeleo kitaaluma mazuri Wanafunzi wote wamefaulu kwenda kidato Cha kwanza amewataka wazazi kupenda shule ya Kimanga darajani kwenda kuwasomesha watoto wao .
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa