Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
JUMUIYA ya Wazazi Kata ya Ilala wamefanya Ziara katika shule za Kata ya Ilala kuangalia changamoto zilizopo katika shule hizo
Ziara hiyo IMEANDALIWA na kamati ya utekelezaji Wazazi Kata ya Ilala ambapo Katibu wa Elimu na Malezi Fridaus sija Jaribu, amefanya ziara hiyo kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sabry Sharif ,Katibu wa Jumuiya Omary Marijan na Viongozi wa matawi .
Akizungumza katika ziara hiyo Katibu wa Elimu na Malezi ambaye anasimamia Elimu wa Wazazi Kata ya Ilala Fridaus Karibu alisema dhumuni la ziara hiyo kuangalia changamoto za shule .
“Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala kwa kushirikiana na Kamati yetu ya Utekelezaji tumeweka utaratibu wa kutembelea shule za Kata yetu kuangalia changamoto mbalimbali ” alisema Jaribu .
Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Ilala Sabry Shariff alisema ZIARA hiyo imetembelea shule tatu shule ya msingi Ilala ,Shule ya msingi Amana na sekondari ya Kasuru.
Mwenyekiti Sabry alisema ZIARA hiyo dhumuni lingine kiwatamburisha Viongozi wa Wazazi katika shule hizo Ili kupokea changamoto ,maendeleo ya shule kufanya kazi kushirikiana na walimu kwa ajili ya kujenga misingi Imara ya Wanafunzi wasimomonyoke kimaadili sekta ya Elimu .
“Ziara hii ni endelevu ya sekta ya Elimu lwa ajili ya kuunga Mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sera ya Elimu Bure “alisema Sabry .
DIWANI wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Aisha Kipini ,alisema Wazazi Wana jukumu kubwa kufatilia sekta ya Elimu kwa kuangalia Maendeleo ya watoto mashuleni hivyo jukumu lao kubwa ni kushirikiana na Walimu waweze kupewa Ushirikiano kujenga nyumba Moja .
More Stories
Hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wanaohatarisha usalama Mbeya
Maofisa ujenzi Manispaa Tabora kikaangoni
Mbeya yapokea bil.23.4 ujenzi sekta ya elimu