January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jumuiya ya Uchumi JUBI wagawa viwanja Homboza

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

JUMUIYA ya uchumi Bora (JUBI )wagawa viwanja kwa wanachama wa Taasisi ya JUBI ili wajiwezeshe kimaisha na kiuchumi.

Akizungumza katika uzinduzi wa Taasisi ya JUBI katibu wa JUBI Mariam Shayo, alisema taasisi hiyo imesajiliwa kisheria mpaka sasa wanachama wao wamenufaika kwa kugaiwa Viwanja vya kujenga nyumba zao Homboza CHANIKA na Wilaya ya Kigamboni.

“Taasisi yetu inaendelea na mchakato wa kigawa viwanja kwa wanachama ambapo kupitia fedha za akiba zao wameweza kukopa na kukuza wigo wake wanachama wa Jumuiya ya Uchumi Bora JUBI sasa hivi wanamiliki viwanja vyao wilaya ya Ilala na nje ya Wilaya Ilala “alisema Shayo.

Katibu Mariam Shayo alitoa wito kwa Serikali taasisi ziwezeshwe iweze kuwafikia walengwa kwani taasisi ya JUBI ina vikundi 20 vya wanawake na wanaume na lika mbali mbali.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya Uchumi Bora JUBI Mariam Kilunga alisema jumuiya hiyo sio ya Kiserikali inajishughulisha na wanawake, vijana pamoja na wananchi wote ambapo jumuiya hiyo imesajiliwa mwaka 2023 kufikia mwaka 2028 Taasisi hiyo itafanya kazi Tanzania Bara yote .

Mkurugenzi Mariam Kilunga alisema Taasisi ya JUBI inashughulika na VICOBA endelevu kauli mbiu yao ” Jubi mafanikio lazima kwa maendeleo ya jamii na kupinga ukatili ” ambapo imefanikiwa kuwaunganisha wanawake wa CHANIKA ,Zingiziwa, Buyuni, Pugu,Segerea na mkoa Dar es Salaam kwa ujumla.

Alitumia fursa hiyo kupomngeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fursa Wanawake waweze kumiliki uchumi na kutafuta fursa mbalimbali za maendeleo.

Aidha alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutunga sera,Sheria na miongozo, juu ya mapambano dhidi ya Umasikini jumuiya hiyo imeweza kuchukua hatua ya pamoja kuwaunganisha pamoja Wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika vikundi na kuweza kuwasaidia ujasiri na kuviwezesha kielimu ili viweze kujiajiri na kupunguza Umasikini katika familia na Taifa kwa ujumla.

Alisema pamoja na jitihada za maendeleo ya Taasisi ya Jumuiya ya uchumi Bora JUBI wameaweza kufanikisha uundwaji wa vikundi 16 kupunguza umasikini baadhi ya wanachama ukiwemo utoaji wa mikopo kupitia vikundi vyao na kuweza kutengeza faida ya vikundi vyote takribani 35,759,000/= pia wamefanikiwa kuanzisha mfuko wa Uwekezaji wa pamoja kwa ajili ya kufanya miradi yao na kuweza kuchanga shilingi milioni 5000,000/=