December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kipawa watakiwa kuanzisha SACCOS na viwanda

Na Heri Shaaban , TimesMajira Online

Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi kata ya Kipawa wametakiwa kuanzisha Umoja wa SACCOS kwa ajili ya kujenga ushirika wao watakaowezesha kukopa na kufanya shughuli zao kukuza uchumi na kuwa wajasiriamali wakubwa.

Akizungumza wakati wa kuzindua Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi kata ya Kipawa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Taifa Fatuma Abdalah Kange, alisema wanawake wa Kipawa wa Jukwaa la wanawake wote ndio watakuwa waanzilishi wa SACOS hiyo .

“Wanawake wezangu wa kipawa mnaweza msirudi nyuma mjikwamue kiuchumi muweze kuwa wajasiriamali wakubwa muanzishe ushirika wa sacos yenu muweze kukopa muwe na mitaji mikubwa itakayowakwamua kiuchumi “alisema Kange.

Fatuma Kange aliwataka Wanawake wa Kipawa kuunda viwanda vya Biashara kupitia ushirika wao kwani wana uwezo mkubwa kupitia jukwaa hilo watafika mbali katika shughuli za ujasiriamali .

Aidha aliwataka watafute masoko ya Biashara ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujenga mtandao wa Biashara zao na kutafuta masoko makubwa .

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Kipawa Saidi Mkuwa, aliwataka wanawake waache nongwa wawe wamoja kujenga ushirikiano katika kukuza Uchumi .

Mwenyekiti Saidi Mkuwa alipongeza Serikali kurudisha majukwaa ya wanawake kwa kuyafufua upya wanawake wajenge umoja wafikie malengo yao ambapo alisema ccm kipawa itasaidiana na wanawake waweze kufikia malengo yao.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake kipawa Ziporah Simwanza alisema kata ya Kipawa ni miongoni mwa kata 36 ndani ya wilaya ya Ilala kila mtaa umeanzisha mradi midogo midogo kwa nguvu zao Wenyewe mtaa Mogo wamejenga mradi wa choo cha kulipia na mradi wa kupika keki jukwaa uwanja Ndege wanatengeza mradi wa vikoi .

Mwenyekiti Ziporah Simwanza alisema kila wakati wanafanya ziara kuangalia uhai wa majukwa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema lengo la kuwa na jukwaa kuwakutanisha wanawake pamoja kuwakwamua kiuchumi kwa kuangalia fursa .

“Alitaja baadhi ya fursa hizo kuwapa elimu ya Bishara na mikopo kuwapa wazo la biashara ,kuwaunganisha na taasisi za fedha,kuwajengea uwezo na kuwaendeleza kibiashara.

Mjasiriamali Maarufu Elizabeth Kilili (GRACE ZOA ZOA)amemshukuru Rais kutenda haki na kuonekana ana hatia yoyote awali Kanisa lilifungwa baada Jeshi la Polisi kumaliza uchunguzi miezi sita amekutwa ana hatia yoyote yupo huru Mama ZOA ZOA anajishughulisha na biashara mbali za vipodozi vya wanawake hapa nchini.

Elizabeth Kilili aliwataka wanawake wawe wabunifu na kuweka BACON bidhaa zao ziweze kutambulika ndani na nje ya nchi kwa kutafuta masoko makubwa