Na Mwandishi Wetu, TimesMajira,Online,Dar
SHULE ya Joyland ya Toangoma jijini Dar es Salaam imeanzisha vilabu mbalimbali kwaajili ya kuvumbua vipaji vya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Hayo yamesemwa shuleni hapo siku ya Jumamosi na Mkuu wa Shule ya Msingi Joyland, Cyprian Maganga wakati wa mahafali ya shule ya awali, msingi na sekondari shuleni hapo.
Amesema wameanzisha klabu ya lugha, hesabu, sayansi, klabu ya uogeleaji, ya mapishi nay a muziki ambapo wanafunzi wenye vipaji wamekuwa wakipata nafasi ya kuonyesha umahiri wao kwenye maeneo hayo.
Amesema mbali na kuwakazania kitaaluma wanafunzi ni vyema shule kuwa na utaratibu wa kuvumbua vipaji vya wanafunzi kama Joylanda inavyofanya ili waweze kuvitumia kwa manufaa yao ya baadaye.
Amesema kwa sasa wanatafuta uwezekano wa kupata chumba cha kufundishia muziki ambacho gharama yake itafikia sh 15,000,000 hivyo aliwaomba wazazi wachangie upatikanaji wa chumba hicho kwa manufaa ya wanafunzi hao.
Amesema katika kuhakikisha Joyland itatoa mchango kwa jamii inasomesha watoto yatima 15 kwenye shule hiyo ambao walikuwa wanalelewa kwenye vituo vya yatima.
Amesema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakijiunza kwa nadharia na vitendo na shule zina kompyuta zisizopungua 60 na kwamba somo la haiba na muziki hufundishwa kwa vitendo na walimu waliobobea kwenye eneo hilo.
Amesema mbali na nadharia wamekuwa wakiwapeleka kusoma kwa vitendo na kwamba hivi karibuni wanatarajia kutembelea mbuga za Mikumi, kidatu, Kihansi, Kilombero Sukari na kwenye milima ya Udzungwa.
“Tunawaomba wazazi wote kuunga mkono ziara hizi za kimasomo ili watoto wenu wapate nafasi ya kujifunza kwa vitendo lakini pia kufanya utalii wa ndani,” amesema Maganga.
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024