November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT yazindua Boti yake kuongeza tija katika ulinzi,uzalishaji

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Kigoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limezindua boti yake ya MV Bulombola ikiwa ni mkakati kabambe wa kufanya uzalishaji mkubwa katika eneo la Kilimo ,mifugo na uvuvi ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kupata ziada lakini pia itatumika katika masuala ya kiusalama ndani ya Ziwa Tanganyika.

Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena ameyasema hayo wakati wa  hafla ya uzinduzi wa boti hiyo katika bandari ya Kigoma.

“Msukumo wa kuitengeneza boti hii ulitokana na mkakati wa kabambe wa JKT wa kuhakikisha kwamba tunakwenda kufanya uzalishaji mkubwa kabisa katika eneo la kilimo,mifugo na uvuvi ,

“Sasa ukiangalia kikosi 821 kipo pembezoni kabisa mwa ziwa Tanganyika ambapo ndani ya Ziwa hilo kuna fursa nyingi sana zikiwemo za usafirishaji ,uvuvi ,maana tunaambiwa ziwa hili ni maarufu sana kwa kutoa samaki aina ya migebuka,kuhe , sangara na dagaa wa Kigoma ,kwa hiyo kufuatia ule mpango wa JKT kuhakikisha kwamba JKT linakwenda kuwa na mapinduzi makubwa hususan kwenye eneo la uvuvi ,

“Tutumie fursa zilizopo kwenyw upande wa bahari,maziwa lakini pia hata katika ufugaji wa matenki na vizimba katika maeneo yetu ya uzalishaji .”amesema Brigedia Jenerali Mabena

Aidha amesema, mpango uliopo baadaye ni kununua boti yenye uwezo zaidi ya hiyo ili kuweza kufanya uzalishaji mkubwa zaidi.

Brigedia Jenerali Mabena ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Kilimo mkakati ,Mifugo na Uvuvi wa JKT  amesema Boti hiyo yenye  uwezo wa kuchukua watu takriban 60 na pia ina uwezo wa kuchukua tani   60 mpaka 80 kwa wakati mmoja ,inaonesha ni kwa namna gani inakwenda   kupunguza tatizo la usafiri kwa watu wanaotumia ziwa Tanganyika kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Pia amesema , inakwenda kuongeza ajira kwani shughuli zitakazofanyika siyo tu zitafanywa na JKT peke yao bali pia zitafanywa na watu wengine huku akisema kiasi cha fesha kitakachopatikana kupitia boti hiyo na shighuli nyingine ,kinapelekwa serikalini kwa ajili ya kuiwezesha serikali katila utekelezaji wa shughuli mbalimbali zenye maslahi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

“Kwa hiyo  mimi niseme tu ,katika ile.mipango tuliyojiwekea tunakwenda kufanikiwa kwa sababu tayari MV Bulombola imekamilika tayari kwa kazi.”amesema Brigedia Jenerali Mabena

Amewataka wahusika wote wanaokihudumia chombo hicho kukifanyia matengenezo kulingana na muda unaotakiwa kitaalam ili kiweze kudumu kwa muda uliokadiriwa.

“Chombo hiki  kinakadiriwa kukaa miaka 25 kitaalam kinaweza kufikisha mpaka umri wa miaka 50 haya yote yatawezekana tu iwapo tutazingatia taratibu za uendeshaji wa chombo hicho,ukifika muda wa kufanya ‘service’ na kila kinachotakiwa kifanyike kwa wakati ili kifuke muda uliokusudiwa uliopangwa.

Mkuu wa  Kikosi 821 Bulombola JKT  Luteni Kanali Juma Hongo amemshukuru   Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda ambaye alifanya ziara kikosini hapo mwaka jana Januari  ambapo walimuhakikishia kwamba walishapata fedha kutoka JKT Makao Makuu  walishapikea fefha kutoka JKT Makao Makuu  kwa ajili ya kusimamia ukarabati wa boti ambayo itakuwa na manufaa mengi ikiwemo uvuvi  na ulinzi katika ukanda wa ziwa Tanganyika.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya HP Marine iliyoifanyia matengenezo boti hiyo Hemed Rashid Hemed amesema kampuni hiyo iliingia   mkataba wa matengenezo ya boti ya Bulombola JKT 821 Agosti 29 , 2022  ambapo alisema tayari wameshakamilidha kazi hiyo.