November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKT kufanya mazungumzo ili vyeti vya mafunzo ya ufundi vya JKT vitambuliwe

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele amesema,Jeshi hilo linawasiliana na Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia ili vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT vyeti vyao vitambuliwe na wizara hiyo.

Amesema,pia JKT linafanya mazungumzo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Kiilimo ili vijana hao waweze kupata fursa zinazopatikana katika wizara hizo zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi hasa katika masuala ya Kilimo na ufugaji.

Meja JenraliRajabu Mabele ameyasema hayo jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utejkelezaji w amajukumu ya Jeshi hilo kwa mwaka 2023/24.

Amesema,pamoja na kujengewa uzalendo Vijana wa JKT wamekuwa wakijifunza mambo mengi kupitia Jeshi hilo yatakayowawezesha kufanya shughuli za kiuchumi na hivyo kuwawezesha kuendesha maisha yao.

Aidha amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 JKT limetengewa na serikali kiasi cha shilingi bilioni 9.96 kwa ajili ya kuendeleza adhma ya kuboresha na kujenga miundombinu makambini.

Kwa mujibu wa Meja Jenerali Mabele pamoja na shughuli nyingine lakini pia fedha hizo zitatumika katika  kuweka miundombinu mizuri katika makambi, pamoja na kuongeza makambi mengine ili vijana wengi zaidi waweze kuchukuliwa .

Vile vile amesema,JKT inaendelea kuboresha vyuo vya ufundi stadi katika makambi ya JKT ili vijana waweze kujengewa stadi mbalimbali watakazozitumia katika kujifutia kipato pindi wanapomaliza mkataba wao na kurejea uraiani.

.

Katika hatua nyingine amesema,mikakati ya Jeshi hilo ni kuhakikisha ifikapo 2024/25 liwe lina uwezo wa kujitosheleza kwa chakula.