December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

JKCI yapata ithibati ya Kimataifa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

MAABARA ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), imepata ithibati ya Kimataifa inayojulikana dunia nzima, vipimo vyake vitakuwa vinaaminika kimataifa, inatarajia kupata vipimo kutoka nchi yoyote hususani kwa wale wanaofanya utafiti mkubwa.

Taarifa hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taasisi hiyo kuvunja rekodi kwa mara nyingine kwa kuaminika kimataifa.

Amesema kuwa ithibati hiyo ilitolewa na Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) , na hiyo imetokana na Shirika la Afya Duniani kuweka taratibu kuhakikisha kwamba vipimo vinavyotolewa viwe vinavyoaminika, kwa hiyo ni lazima upate ithibati (accreditation).

“Taasisi yetu kwa mara nyingine inaandika historia kwa maabara yetu inahudumia wagonjwa moyo na wagonjwa wengine, imepata ithibati ya kimataifa, hii inamaana kwamba maabara inaaminika katika vipimo vikubwa kwa kuwapima wagonjwa na katika utafiti,”amesema Dk Kisenge

Pia, amemshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha taasisi hiyo, kwa sababu wanapokuja wakaguzi kufanya ukaguzi wanaangalia eneo,watu wanaofanya hivyo vipimo, lakini pia wanaangalia vifaa na mambo mengine mbalimbali.

“Ni kitu ambacho ni kigumu sana maabara nyingi za hapa Afrika na Katibhazipati ithibati, kwa hiyo kweli sisi kama nchi tumeandika historia kubwa. Vipimo vyetu ambavyo tutakuwa tunavitoa nchi yoyote inaweza kuleta vipimo vyake hapa na hii itakuwa ya mafanikio kwa sababu mapato kitaongezeka,”

“Haya mapato yanaweza kuwarudia wananchi wa hali ya chininambao hawana uwezowa kulipia vipimo, na wengine unakuta upasuaji wake unagaharimu sh milioni 80, kwa hiyo tunachukua fedha hizo kwa kumsaidia ili apate huduma,”amesema

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Maabara hiyo, Emmanuel Mgao amesema wanayofuraha kwa kukidhi viwango vya kimataifa katika kutoa huduma za maabara, haikuwa kazi rahisi walipitia hatua nyingi hadi kufanikisha hilo kwa ushirikiano mkubwa wa wafanyakazi wa maabara hiyo.

“Tukiangalia toka maabara hii imeanza tangu mwaka 2018 mpaka sasa ni miaka sita imeweza kukidhi viwango licha ya kwamba kulikuwa na hatua mbalimbali za kufuata hadi kufikia walipo na kufanikiwa kupata ithibati,”amesema