Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga limepitisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Jiji kwa mwaka 2022/2023 ya kiasi cha shillingi Billion 73 ambazo zitatokana na mapato ya vyanzo vya ndani, ruzuku na wahisani.
Bajeti hiyo imepitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la Halmashauri ya Jiji hilo.
Akizungumza baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amesema bajeti hiyo imeguswa maeneo yote muhimu kwa maendeleo ya jiji la Tanga.
Katika kikao hichoMeya Shiloo alisema kwa upande wa mapato ya vyanzo vya ndani, Halmashauri imekadiria kukusanya kiasi cha shillingi Billion 16, huku nguvu za wananchi katika uchangiaji wa miradi ya maendeleo zikikadiriwa kuwa shillingi Million 824.6, huku fedha za kutoka Serikali kuu na wahisani zikikadiriwa kuwa shillingi Billion 56.
Mpango wa Maendeleo katika mwaka 2022/2023 Halmashauri imekasimia kutumia jumla ya shillingi Billion 19.9 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo Billion 13.1 ni fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na wahisani, na shillingi Billion 6.7 ni fedha za mapato ya ndani na nguvu za wananchi na michango ya fedha taslim makadirio yakiwa ni million 824.
Halmashauri itatumia Billion 6.7 za mapato ya ndani kwa mwaka 2022/2023 katika utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na Mfuko wa utoaji mikopo ya wanawake, vijana na wenye ulemavu kiasi cha sh. Billion 1.2, Ujenzi wa barabara za lami kupitia Tarura sh. Billion 1.2,ukarabati wa kituo cha Afya Pongwe.
Miradi mingine ni Ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shule za Msingi na Sekondari, Ukarabati wa masoko ya Makorola, Kisosora na Majengo, Ujenzi wa nyumba za watumishi, Ukamilishaji wa vyumba vya maabara katika shule za Sekondari.
Aliendelea kuitaja miradi hiyo kuwa ni Ujenzi soko la samaki Deep Sea, uwezeshaji wa kituo cha Tanga TV, Ujenzi wa shule mpya ya Msingi ya English Medium, Kupima viwanja 500 kwenye maeneo ya Amboni, Tongoni, Mabokweni na Ndaoya.
Na miradi mingineyo.
Meya Shiloo alisema Halmashauri hiyo pia imetenga fedha za uendeshaji wa ofisi za Kata na za Mitaa, ambapo kiasi cha shillingi Million 20 kitatolewa kila baada ya miezi mitatu katika kata zote 27, na kiasi cha shillingi 200,000.00 kimetengwa kutolewa kwa kila mtaa kwa kila robo mwaka.
Kwa upande wao madiwani wa halmashauri ya jiji hilo wamesema bajeti hiyo haikuwa na mpinzani kwa kuwa kila diwani alikuwa ameridhika kwa namna ambavyo bajeti hiyo inakwenda kutatua changamoto za maeneo yao.
Katika bajeti ya mwaka 2020/21 Halmashauri ya Jiji la Tanga ilikusanya zaidi ya bilioni 54 sawa na asilimia 79 ya makisio ya bajeti ya mwaka ya zaidi ya shilingi bilioni 68.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato