January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi Kilimanjaro la lafanya usafi Maeneo mbalimbali ya Manisapaa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro katika kuhakikisha wanashiriki pamaja na wananchi Mkoani humo limeshiriki na kufanya usafi kwa pamoja na wananchi ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko.

Akiongea katika zoezi hilo Kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON MAIGWA amesema wao kama Jeshi la Polisi Mkoa Kilimanjaro wameona ni vyema kushirikiana na jamii katika shughuli za usafi wa mazingira ili kuwa na Jamii inayoishi katika mazingira safi na salama.

Kamanda Maigwa amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu Mkoani humo.Sambamba na hilo kamanda Maigwa amewaomba wafanyabiashara wa eneo la soko hilo kuwa na utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara ili kuepuka magonjwa ya milipuko.

Kwa upande wake kaimu Mkurungenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi Sifael Kulanga amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kushiriki pamoja na wananchi katika shughuli za kijamii.

Vile vile ameliomba Jeshi la Polisi mkoani humo kuendelea na utamaduni huo wa kushirikiana na wananchi ili kujenga umoja na ushirikiano baina ya Jeshi hilo na wananchi.