January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi Gongolamboto lapiga marufuku vigodoro kukesha

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online Ilala

JESHI la Polisi Kata ya Gongolamboto limepiga marufuku vingoma vya Mtaani maarufu vigodoro kukesha katika kata ya Gongolamboto kwa ajili ya Usalama wa raia na mali zao.

Jeshi la Polisi limeagiza Wananchi wote wenye shughuli za vigodoro waanze sasubuhi mpaka Jioni wawe wamemaliza Shughuli watakao kaidi agizo watachukuliwa hatua na Jeshi la Polisi.

Akizungumza katika mkutano wa Serikali za Mtaa Ulongoni Gongolamboto ulioandaliwa na Mwenyekiti Abdulrahim Munisi OCD wa Gongolamboto A/ISP Charles Kishai alisema katika kata hiyo Shughuli za vigodoro zinatakiwa kuanza asubuhi mpaka jioni na shughuli za ukumbini mwisho saa sita usiku .

OCD Charles alisema wananchi wengi wameweka utaratibu wa kukesha na vigodoro mitaani jeshi la polisi litawakamata wote watakaovunja Sheria na taratibu .

“Tunawaomba Wananchi wote wenye shughuli kufuata utaratibu Serikali za Mitaa ili uweze kupewa kibali “alisema OCD Charles.

Akizungumzia Ulinzi na Usalama amewataka apewe Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi Ikiwemo kupewa taarifa za siri bila kusingiziana kesi .

Aliwataka Wananchi wa Ulongoni kutoa taarifa za uharifu ikiwemo kutunza Siri za uharifu sambamba na kulipa tozo ya Ulinzi Shirikishi .

Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Ulongoni Kata Gongolamboto Abdulrahim Munisi aliwataka wananchi watoe tozo kwani ukitoa tozo sawa umelindaMwenyekiti Munisi alisema suala la Ulinzi shirikishi lipo kisheria amewataka Wananchi walipe tozo ya Ulinzi kukwepa kifungo .

Aidha alisema Mwananchi ukikamatwa ujatoa tozo ya Ulinzi sawa na muharifu hivyo utachukuliwa hatua za kisheria .