January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jerry Slaa akiwasili Bungeni kuhojiwa na Kamati ya Bunge

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa akiwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuitikia wito wa Spika Job Ndugai wakumtaka kufika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge. Aliwasili jana katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa (katikati) akisindikizwa na Maaskari wa Bunge wakati alipowasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuitikia wito wa Mhe. Spika Job Ndugai wa kufika mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge, jana katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa akipita kwenye mashine kwa ajili ya ukaguzi wakati alipowasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya kuitikia wito wa Mhe. Spika Job Ndugai ya kufika mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya Bunge leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma