Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ukonga ndugu Jerry Silaa kabla amewaona wananchi wa Jimbo la Ukonga,kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani kimedhamiria kuwaletea maendeleo zaidi ambayo baadhi tayari Rais John Magaufuli ameyafanya.
Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mongolandege Kata ya Ukonga, Jerry amesema kuwa CCM endapo watamchagua kuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga atashirikiana na viongozi katika kutatua kero kubwa ya daraja ambalo wakazi hupata kero kubwa hasa kipindi cha mvua kutokana na kutopitika kwa muda mrefu.
“Ninawaomba mnichague mimi nilikuiwa diwani kwa kipindi cha miaka 10 mengi nilifanya na mmeyaona hivyo ninawaomba tena mnichague katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu kwa kuanza kura za Rais John Magufuli, ubunge na udiwani,” amesema.
Amesema kuwa mbali ya kero hiyo pia atahakikisha kuwa zahanati ya Mongolandege inapandishwa hadi na kuwa kituo cha afya kwani tangu kipindi cha uongozi wake kituo hicho hakijapandishwa hadhi hivyo ni vyema wakampa kura nafasi ya ubunge ili afanikishe matarajio yake mengi.
“Kuna mengi ambayo nataka kuyafanya hivyo nawaomba mnipe kura pamoja na diwani anayewania Kata ya Ukonga Ramadhani Bendera ili tuzungumze na kuelewana na kufanikisha maendeleo,” amesema.
Wakati huo huo, Jery amewaomba wakazi wa Kata ya Kitunda kuhakikisha kuwa wanakichagua Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili kero wanazokabiliwa nazo zipatiwe ufumbuzi.
Akizungumza katika ufunguzi wa kampeni katika kata hiyo iliyofanyika Mtaa kwa Mtaa kuomba kura amesema kuwa anatambua kuwa wafanyabiashara wana changamoto nying hivyo endapo watamchagua atahakikisha kuwa anashirikiana na Rais Magufuli pamoja na diwani wa eneo hilo kuzitatua.
Amewaomba wananchi wa kata hiyo ifikapo Oktoba waichague CCM kwa kura za kishindo kwani maendeleo yaliyofanyika ni utekelezaji wa sera na ilani ya CCM hivyo bado kuna mengi ambayo yanatarajiwa kufanyika.
“WanaKitunda ninawaomba nafasi ya urais,ubunge, udiwani mtupe CCM ili tuendeleee kuleta maendeleo ambayo kwa muda mrefu mmekuwa mkisubiri,’ amasema.
More Stories
RC Mtambi awataka Maofisa kilimo kutoa elimu ya kilimo mseto
Rais Samia kuelekea nchini Brazil kushiriki mkutano wa G20
Rais Samia atoa maagizo ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo