December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jamii yatakiwa kuondokana na imani potofu kuhusu sikoseli

Na Penina Malundo,Timesmajira. Online

MWENYEKITI na Muasisi wa Taasisi ya Wagonjwa wa Selimundu Tanzania, Arafa Salim Said ameiomba serikali kuhakikisha vipimo vya Selimundu(sikoseli )vinapatikana katika Mikoa yote nchini na kuruhusu dawa za Hydroxyurea kupatikana katika vifurushi vyote vya Bima ya Afya kwa wagonjwa wanaougua ugonjwa wa sikoseli.

Akizungumza leo katika Tamasha la Mashujaa wa Sikoseli lililoandaliwa na Sickle Cell Disease Patient Community of Tanzania kwa udhamini wa Taasisi ya Novo Nordisk Haemphilia Foundation,amesema kama Taasisi wanazidi kuomba serikali kuhakikisha watu wanapimwa mapema ili wajitambue afya zao.

“Tunatambua serikali inamikakati mikubwa katika hili lakini kama Taasisi tunaomba serikali irahisishe upatikanaji wa vipimo na dawa za Hydroxyurea ziweze kupatikana kwa urahisi katika vifurushi vyote vya Bima ya afya ya NHIF ili watu waweze kupata kwa urahisi na gharama nafuu,”alisema

Aidha amesema tangu kuanzisha kwa Taasisi yao miaka 11 hadi sasa wanawatoto 300 ambao wanawasaidia katika Taasisi yao na bado wanaendelea kutafuta watoto wengine kuwasaidia.

“Taasisi yetu inatoa elimu na kusaidia watu wanaoishi na sikoseli kupata elimu na kujitambua zaidi hivyo leo tumeshiriki wanadar es Salaam katika kutambua vipaji vyao na kuendele kutoa elimu nchini juu ya ugonjwa huo,”amesema