Jaji Mutungi aongoza kikao cha TCD
Na Agnes Alcardo TimesmajiraOnline,Dar
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, leo Agosti 18, 2024 Jijini Dar es Salaam, ameongoza Kikao cha Mashauriano cha Vyama vya Siasa Wanachama wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambacho mbali ya viongozi wa vyama hivyo, pia kimehudhuriwa na Mawaziri na Manaibu waziri wakiwakilisha upande wa Serikali.
Baadhi ya viongozi wakuu wa vyama hivyo walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Mwenyekiti wa TCD kwa sasa, Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR- Mageuzi, Joseph Selasini.
Aidha kwa upande wa Serikali, umewakilishwa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, aliyemwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Festo Ndugange, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Daniel Sillo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito