January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jaji Dkt. Yose: Huduma za Hifadhi ya Jamii ni Haki ya Kikatiba

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina, akitoa hotuba ya kufunga kikao kazi cha siku mbili kilichowaleta pamoja Majaji na Watendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Ziwa na Wakurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA). Wengine pichani katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Mwanza, Mhe. Dkt. Ntemi Kelekamajenga, na Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini,  WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar. 

Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine, alisema  “Huduma za Hifadhi ya Jamii ni Haki ya Kikatiba, kwa mujibu wa Ibara ya 11, ibara ndogo ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorejewa mara kadhaa. Serikali inao wajibu wa kuweka mazingira ya kisera na kisheria kwa lengo la kuhakikisha pamoja na mambo mengine kila mwananchi anapata kinga wakati wa uzee, ugonjwa au ulemavu na kwa kuzingatia matakwa ya katiba, serikali iliona ipo haja ya kutunga sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura ya 263.” Alisema.

Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini,  WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza mwishoni mwa kikao kazi cha siku mbili kilichowaleta pamoja Majaji na Watendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Ziwa na Wakurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

 Pamoja na ammbo mengine Dkt. Omar aliwashukuru Waheshimiwa Majaji na Watendaji wote wa Mahakama Kanda ya Ziwa na Wakurugezni wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA kwa kushiriki katika kikao kazi hicho cha pili kuwahusisha Majaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, kikao cha kwanza kilifanyika Juni 9, 2023 mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani. “Mfuko utaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali na mafunzo kama hayo yatakuwa ni endelevu ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wafanyakazi ambao ndio walengwa wakuu wa Mfuko.” Alisema Dkt. Omar.

Dkt. Omar akimpongeza Mhe. Dkt. Mlyambina baada ya kufunga kikao kazi hicho.

Jaji Mfawidhi wa Mwanza, Mhe. Dkt. Ntemi Kelekamajenga (mbele) na Waheshimiwa majaji wengine wakisikiliza hotuba ya kufunga kikao kazi.

Waheshimiwa Majaji na washiriki wengine wakifuatilia hotuba ya kufunga kikao kazi

Waheshimiwa Majaji na washiriki wengine wakifuatilia hotuba ya kufunga kikao kazi

Mhe. Jaji na washiriki wengine wakati  wa hafla ya kufunga kikao kazi