November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Islamic Education Panel yatangaza matokeo mtihani wa dini

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Taasisi ya Islamic Education Panel, imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya Kiislamu na lugha ya kiarabu, uliofanyika Agosti 9, mwaka huu, pamoja na mtihani wa kuhitimu Madrasa uliofanyika Agosti 12,13 2023.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, mjumbe wa taasisi hiyo taifa, Mussa Yusufu Kundecha amesema jumla ya shule 3975 kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na Visiwa viwili vya Zanzibar (Unguja na Pemba), zilishiriki mtihani huo.

“Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa somo la dini ya Kiislamu walikuwa 174,719, watahiniwa waliofanya mtiahani ni 157,823 sawa na asilimia 90.33.

“Idadi ya watahiniwa ambao hawakufanya mtihani mtihani kutokana na sababu mbalimbali walikuwa 16,896, sawa na asilimia 9.67,” amesema Kundecha.

Hata hivyo amesema, idadi ya watahaniwa waliofanya mtihani imeongezeka kwa watahiniwa 6878 sawa na asilimia 4.56 kutoka watahiniwa 150,945 mwaka 2022 hadi watahiniwa 157,823 mwaka 2023.

Amesema, hiyo inatokana na idadi ya shule kuongezeka kutoka 3,903 mwaka 2022 hadi 3975 mwaka 2023, ambayo sawa na ongezeko la asilimia 1.8.

Kundecha amesema, mtihani waliofanya watahiniwa hao ulikuwa na jumla ya alama 50, matokeo yalitolewa kwa madaraja A hadi E. Ambapo mtahiniwa anahesabika kwa ufaulu akiwa amepata daraja A,B,C au D.

“Idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupata madaraja A hadi D ni, 139,181 sawa na asilimia 88.19 ya watahiniwa wote 157,823.Idadi ya watahiniwa waliopata daraja E ni, 18,591 sawa na asilimia 11.81 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani,” amesema.

Aidha, Kundecha amezitaja shule 10 bora zilizofanya vizuri kitaifa zenye watahiniwa 20 au zaidi.

1.Mbagala Islamic Primary Shool iliyopo Manispaa ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam yenye wastani 49.33.

  1. Muzdalifa Islamic Primary Shool, Nachingwea mkoani Lindi ina wasatni 49.08.
  2. Ibun Jazar Primary School, Mkuranga mkoa wa Pwani yenye wastani 48.48.
  3. Mumtaaz Primary School, Jiji la Mwanza wakiwa na wastani wa 46.77.
  4. Bismarck Primary Shool, Manispaa ya Ilemela, Mwanza wana wastani 46.65.
  5. Rahma Primary School, Dodoma ina wastani 46.62.
  6. Kanga Primary School, Mafia mkoa wa Pwani wakiwa na wastani wa 46.03.
  7. Algebra Islamic Primary School, Kigamboni, Dar es Salaam wastani wake ni 46.03
  8. Kyenge Islamic Primary School, Bukoba, Kagera wastani wake 45.88.
  9. Muzdalifa Primary School, Masasi, Mtwara wasatini wake 45.71.

Mbali na hivyo, pia Kundecha ametaja mikoa yenye ufaulu wa juu Tanzania Bara na visiwani kuwa ni.

  1. Kisiwa cha Pemba, wastani 33.85.
  2. Kisiwa cha Unguja, Wastani 24.25.
  3. Dar es Salaam, Wastani 21.95.
  4. Kagera, Wastani 21.19.
  5. Arusha, Wastani 20.81.
  6. Pwani, Wastani 20.16.
  7. Songwe, Wastani 19.85.
  8. Rukwa, Wastani 18.94.
  9. Morogoro, Wastani 18.65.
Mjumbe wa Taasisi ya Islamic Education Panel, Mussa Yusufu Kundecha (katikati), akitangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya Kiislamu na lugha ya kiarabu, uliofanyika Agosti 9, mwaka huu, pamoja na mtihani wa kuhitimu Madrasa uliofanyika Agosti 12,13 2023, mbele ya Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam pichani hawapo. Na Mpigapicha Wetu