Na Esther Macha,TimesmajiraOnline, Mbeya
WIZARA ya maji imesema wastani wa vijiji 9,670 nchini kati ya vijiji 12,318 vimefikishiwa huduma ya maji safi na salama ambayo ni sawa na asilimia 77 ikilinganishwa na asilimia 88 ya wananchi waishio mijini na vijijini.
Imeelezwa kuwa mikakati ya Wizara kuhakikisha ifikapo 2025 asilimia 85 maeneo ya vijijini na asilimia 95 ya maeneo ya mijini watakua wamefikishiwa huduma hiyo lengo ni Serikali ya awamu ya sita ni kumtua Mma ndoo kichwani.
Sambamba na hatua hiyo kubwa serikali inaendelea kuboresha huduma ya maji licha ya baadhi maeneo kukabiliwa na changamoto hiyo sambamba na Serikali kutekelezwa kwa gharama kubwa .
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 28,2023 na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya ,Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati wa ufunguzi wa kongamano la maji la mwaka 2023(ATAWAC 2022)ambalo linafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Eden uliopo mkoani hapa.
Mhandisi Mahundi amesema kuwa kutokana vipaumbele vya serikali kuwa vingi kazi zinaendelea na lengo ni kuhakikisha juhudi mbali mbali zinafanywa na zaidi kushirikisha sekta binafsi katika kuboresha sekta ya maji kwenye maeneo yote yenye huduma ikiwemo kwenye vyanzo vyote vya maji uzalishaji na usambazaji wa maji na utawala wa fedha .
“Haya yote tunafanya kwa dhamira kwamba maeneo ambayo hajafikiwa na yenyewe pia lazima yafikiwe hii ndo dhamira ya wizara , namo mwaka 2018 wizara ya maji na umwagiliaji ikishirikiana na wizara viwanda na biashara ,wadau wa sekta binafsi na mashirika ya maendeleo waliingia makubaliano kwa namna bora ya kushirikisha sekta binafsi kuchangia katika kuboresha sekta ya maji nchini na makubaliano hayo yaliwezesha wizara ya maji kutengeneza mpango kazi wa miaka mitano mwaka 2018 mpaka 2025.
Aidha Mhandisi Mahundi amesema kuwa kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo kutafungua miradi mingi ya maji ya ushirikano na wizara itafunguka na miradi kuongezeka zaidi ili kuboresha huduma ya maji nchini .
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema kongamano hilo lina umuhimu mkubwa kwani sekta ya maji ina mchango katika kuhakikisha pato la nchi linaongozeka kupitia viwanda na sekta zingine .
Mhandisi Mahundi ameeleza kuwa wizara ya maji itaendelea kuboresha sera na sheria zake ili ziweze kuwa rafiki kwa wadau na wawekezaji wote nchini na kutoa wito kwa wadau wa sekta binafsi kujiandaa kutumia fursa ya kuwekeza katika sekta ya maji kupitia milango ambayo serikali imefungua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Jijini Mbeya , Bi Edina Mwaigomole amesema kuwa wanatambua kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na wizara ya maji na wadau na sekta binafsi .
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu