December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ilala yatajwa kuwa Mwenyekiti Bora wa Hajji

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde , amesema katika wilaya ya Ilala yenye mitaa 159 Mwenyekiti bora wa Serikali za mitaa, anayeteleza ilani kwa vitendo Hajji Bechina ambapo anafanya kazi za chama na kijami,kwa kushirikiana na serikali.

Mwenyekiti Sidde alisema hayo kata ya Ilala mtaa wa Karume wakati wa mkutano wa kuwasilisha utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2019 /2024 taarifa iliyowashirishwa na Mwenyekiti Bechina.

“CCM wilaya ya Ilala inatoa pongezi kubwa kwa Mwenyekiti Bechina anayejituma katika utekelezaji wa majukumu yake, na utekelezaji wa Ilani ya chama mtaa wa Karume amefanya mambo makubwa Mwenyekiti wa kwanza anayejua uongozi na kutekeleza Ilani ya chama na kuisaidia jamii ikiwemo kulisha chakula kila mwaka shule za Ilala Boma na Mkoani pamoja na kutoa meza za Walimu katika shule hizo kila wakati kwa kushirikisha wadau”alisema Sidde.

Mwenyekiti Sidde amesema FOMU ya kugombea Mwenyekiti Hajji Bechina ikifika katika mkono wake ataitendea vyema kutokana na jitihada zake za utendaji kazi kwenye maeneo ya Mtaa wake wa Karume na kuwa karibu na Jamii.

Aliwataka wana CCM kushirikiana na kujenga mshikamano na mahusiano bora kwani CCM ina nafasi nyingi za uongozi hivyo kila kiongozi amepangiwa nafasi yake kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kata ya Ilala kuna uongozi bora.

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu alisema Mwenyekiti Hajji Bechina mtu anayejitoa na ni kiongozi bora kwani kiongozi bora sio pesa ni kujituma .

Aliwataka wana Ilala kushirikiana pamoja katika kujenga chama na Serikali na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta maendeleo na miradi mikubwa ya maendeleo.

Mbunge Zungu aliwataka wananchi wa jimbo la Ilala wasiuze nyumba hivi karibuni barabara zote zitajengwa za ndani na kukamilika majumba ya Ilala yatapanda thamani kubwa wakati mwingine kuchelewa kwa ujenzi sio suala la Wakandarasi mifumo inachelewa hivyo wananchi wawe wasikivu Serikali inafanya kazi .

Kada wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Alu Segamba alisema Mbunge Mussa Zungu anatosha Ilala na Mwenyekiti Hajji Bechina anatosha Mtaa wa Karume kwani chama chetu kina fitina na majungu kiongozi mchapa kazi fitina na majungu lazima yamkute.

Kada Segamba alisema Mbunge Zungu,Diwani Saady Khimji na Mwenyekiti Bechina anarusiwa kufanya chochote eneo lake tofauti na mtu mwingine kwa ajili ya kutekeleza Ilani ya chama na kutatua kero mbali mbali za wananchi.

Aliwataka wana CCM wawe na nidhamu na kuzingatia muda wa vikao vya uteuzi pia mgombea wa CCM ajiuze Mwenyewe aina haja kujiuza