Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
ALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam wameunda kikosi cha wachezaji 120 kwa ajili ya Mashindano ya Umoja wa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) Kanda ya Dar es Salaam.Wachezaji hao 120 Wameweka kambi yao ya siku kumi shule Kabby Academy iliyopo Ukonga Wilaya ya Ilala.
Akizungumza katika kufunga mashindano ya ngazi ya Wilaya llala Iliyoshirikisha Klasta nne za Halmashauri ya Jiji Kaimu Afisa Michezo Halmashauri hiyo ASHA MAPUNDA alisema wachezaji wote 120 wana afya nzuri leo wameanza kambi rasmi baada kumaliza michezo ngazi ya Wilaya ambapo katika timu zote tumechuja tumeweza kupata wachezaji wote 120 katika michezo mbalimbali watakuwa katika uangalizi Maalum.
“Timu yetu ya Halmashauri ya Jiji imejipanga vizuri kwa ajili ya kuchukua ubingwa tena mwaka huu tunaingiza wachezaji uwanjani tunatetea ubingwa wetu miaka minne yote Wilaya ya Ilala tumekuwa mabingwa na mwaka huu tunachukua kombe la Kanda ya Dar es Salaam” alisema Asha.
Asha alisema katika mashindano ya Kanda ya Dar es Salaam wanakutana na Wilaya ya Kinondoni,Temeke,Ubungo,na Kigamboni kutafuta timu moja itakayowakirisha Dar es Salaam mashindano ya ngazi ya Taifa yatakayofanyika Tabora mwaka huu.
Alisema katika wachezaji 120 wa Ilala waliounda leo baadhi yao wachezaji wa soka la Wanawake na Wanaume, Netboli,kwaya,Ngoma, ,riadha Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Jiji,Abirah Nchia, alisema lengo kuu la mashindano hayo ngazi ya Wilaya kuibua vipaji vya michezo mbalimbali na kutambua wana michezo mahiri zikiwemo fani za ndani .
Mwalimu Nchia alisema michezo ina faida nyingi ikiwemo kujenga Afya ya mwili kiakili, kiuchumi, ambapo watu upata ajira kupitia michezo pia uleta furaha na upendo.
Aidha alisema mashindano ya UMITASHUMTA mwaka huu 2022 imebeba ujumbe Maalum usemao.
Akizungumza changamoto alisema ya timu ya Kambi ya Ilala alisema ukosefu wa vifaa vya michezo ikiwemo viatu ,Jezi,mipira,vifaa vya riaadha kama tufe,mkuki,kisahani, pamoja na mipira ya kengele.
Akizungumzia changamoto nyingine Chakula kwa ajili ya Kambi, Maji na vinywaji.
Akizungumza katika mashindano hayo Mkurugenzi wa Raslimali Watu na Uendeshaji Benki Kuu ( BOT )Kened Nyoni aliyemwakilisha GAVANA wa Benki Kuu Tanzania aliwapongeza Ilala kuwa vinara wa Michezo hiyo UMITASHUMTA Mkoa wa Dar Salaam waendelee kufanya vizuri zaidi Katika michezo yao.
Kened Nyoni alisema kwa niaba ya Benki Kuu BOT wamekubali kusaidia michezo Ilala amewataka wasimamie timu vizuri wasishie hapo kwani michezo inasaidia akili kukua pamoja na kukuza taaluma shuleni.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa