Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MBUNGE wa Jimbo la Ilala, ambaye ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, amesema Jimbo la Ilala linatarajia kuibua vipaji vya wachezaji wa timu ya Taifa.
Mbunge Zungu alisema hayo jimbo la Ilala wakati wa kugawa mipira kwa ajili ya sekta ya michezo vilivyotolewa na Lion clubs katika maadhimisho ya wiki ya huduma Duniani.
“Tunashukuru msaada huu Lion Clubs ni wezetu kwa ajili ya kugawa shule zetu zote za jimbo la Ilala za msingi na Sekondari mikakati yetu kuibua vipaji wachezaji bora wa timu ya Taifa ” alisema Zungu.
Mbunge Zungu alisema mwili ukiwa na afya unafanya vizuri kutokana na mazoezi amewataka watumie mipira hiyo katika sekta ya Michezo katika shule zao.
Aliwapongeza viwango vya ufaulu kuongezeka katika shule za Jimbo la Ilala wanafunzi wanafaulu vizuri kutokana na taaluma kukuwa katika shule hizo kutokana na ushirikiano wa Wazazi na walimu .
Diwani wa Kata ya Upanga Mashariki Sultan Salim, alishukuru kwa msaada huo Lion Clubs, kuisaidia Serikali jimbo la Ilala katika sekta ya Michezo waweze kutengeza timu kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari kwa ajili ya kutengeza vipaji waweze kuja saidia Taifa.
Diwani Sultan Salim, aliwapongeza waratibu wa siku hiyo ya maadhimisho ya siku ya Huduma za Jamii amewataka siku nyingine awasaidie maswala mengine ya kijamii.
Mratibu wa maadhimisho ya siku ya Huduma Duniani ambaye ameandaa hafla hiyo Happiness Nkya, alisema taasisi ya Lion Clubs inajishughulisha na maswala ya jamii ambapo katika kuadhimisha siku hiyo imejitolea kutoa zawadi ya mipira kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari zilizopo jimbo la Ilala baada kuona michezo kwa wanafunzi ni chachu kubwa ya kumfanya mwanafunzi kua imara kiakili , Kimwili na Kiafya.
Happiness Nkya alisema Lion Clubs imepata ufadhiri huo kutoka kwa kiongozi aliyepita ambaye kwa sasa ni Marehemu imekuwa sehemu ya kumuenzi kiongozi huyo kwa kile ambacho alikuwa anafanya enzi za uwai wake .
More Stories
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto
Jela miezi sita kwa kuvaa sare za JWTZ
Watolewa hofu uvumi juu ya uwepo wa Teleza