Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana inatarajia kufanya kampeni ya RAFIKI wa AMANA, ambayo inalenga kukusanya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Hospitali ya mkoa kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati(NJITI).
Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mkuu Mfawidhi wa Rufaa Amana Dkt.Bryceson Kiwelu ,alisema Agosti 17 mwaka huu kutakuwa na matembezi ya Hisani yenye lengo la kuboresha miundombinu kuanzia ujenzi wa Wodi ya mama na mtoto pamoja na ununuzi wa vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kisasa vya watoto njiti.
“Hospitali ya Rufaa Amana inatarajia kufanya kampeni ya RAFIKI wa AMANA ambayo inalenga kukusanya bilioni 3 kwa ajili ya watoto kuboresha miundombinu ya watoto waliozaliwa kabla wakati “alisema Dkt. KIWELU
Dkt. Kwelu alisema kampeni hiyo itaitimishwa kwa chakula cha hisani katika ukumbi wa Mlimani City Agosti 31 mwaka huu 2024 ambapo kitahusisha wadau mbalimbali wenye mapenzi mema na Hospitali ya Amana.
Aidha aliwataka wadau mbalimbali kuhitokeza kwa wingi katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya afya kuweka mazingira bora katika wodi ya watoto njiti .
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM