December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hospital ya Mawenzi yaadhimisha miaka 99 kwa kutoa huduma Bure

Na Martha Fatael, TimesMajira Online

WAKAZI zaidi ya 4,000 mkoani Kilimanjaro wanatarajiwa kufanyiwa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani ya tenzi dume na shingo ya kizazi bila malipo katika kuadhimisha Miaka 99 ya hosptali ya Mawenzi sambamba na kusherekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.

Mganga mfawidhi wa hosptali ya Mawenzi, Dk Edina-Joy Munisi, ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mahadhimisho ya wiki ya Mawenzi, yaliyoenda sambambamba na kusherekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania, yaliofanyika katika viwanja vya uhuru Park, Mjini Moshi, mkoani hapa.

Amesema huduma za vipimo vya Bure imefanyika kwa magonjwa ya sukari, saratani ya shingo ya kizazi, shinikizo la damu, uzito, macho, damu kubwa na magonjwa mengine ambapo kwa siku ya kwanza Disemba 08 walitoa huduma kwa wananchi 2,000 na Disemba 09 walitoa huduma kwa wananchi 2,000 na kwamba matibabu na vipimo vilivyotolewa ni uchunguzi wa tenzi dume,saratani ya shingo ya kizazi pamoja na utoaji wa chanzo za ugonjwa wa homa ya ini na Uviko19.

Aidha amesema zoezi hilo linaongozwa na jopo la madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ambapo watafanya uchunguzi wa kina kwa kutumia vifaa ambavyo hutumika hospitalini hapo.

“tumehadhimisha wiki ya mawenzi ambayo imeanza kuanzia Disemba 06 na tutahitimisha Disemba 10 mwaka huu, tumefanya mambo mbalimbali kama kuwafikishia huduma wananchi wenzetu waliopo magerezani pamoja na kutoa matibabu na vipimo bure kwa wananchi ambapo tumekadria watafika 4000”amesema Dk. Munisi

Kwa upande wake, Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Gradianus Mgimba, amesema katika kipindi cha kuhadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania na miaka 99 ya hosptali hiyo, inajivunia mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma bora za afya ambazo zimekuwa chachu ya maendeleo.

Aidha amesema baada ya maadhimisho hayo huduma hizo zitaendelea kutolea kwa wananchi katika hosptali hiyo na kwamba wananchi wanawajibu wa kujijengea utamaduni wa kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kuepukana na usugu wamagonjwa ambao unaweza kuepukika.

Awali Mratibu wa huduma za tiba wa hosptali hiyo, ,Dk. Emanuel Irira, amesema licha ya kuhadhimisha miaka 99 ya hosptali hiyo na miaka 60 ya uhuru, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upungufu wa vifaa na madaktari bingwa katika magonjwa mbalimbali ikiwemo eneo la upasuaji na daktari bigwa hususan magonjwa ya wanawake.