January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hekari 535 za mirungi zateketezwa

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

Hekari 535 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa katika oparesheni maalum ‘Tokomeza Mirungi’, iliyoanzia kutekelezwa ndani ya Vijiji vya Rikweni, Heikondi, Tae na Mahande, WIlayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro kwa muda wa siku nane kuanzia Julai 2 hadi 9,2023.

Oparesheni hiyo inafanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ikishirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama likiwamo Jeshi la Polisi Tanzania.

Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo amesema katika oparesheni hiyo jumla ya Watuhumiwa saba wamekamatwa huku akisema mirungi ni moja ya dawa za kulevya zilizokatazwa nchini kwani ina athari nyingi kwa binadamu, kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiafya.

“Inasababisha saratani ya koo, utumbo na uraibu, mtindio wa ubongo, kiuchumi inasababisha Nchi inakosa mapato kwasababu wengi wanaolima mirungi Kata hii na eneo hili la Same hawaingizii mapato yoyote Serikali”

“Nawashukuru wote ambao tunashirikiana nao katika oparesheni hii, tuwaombe Wananchi wote kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan, Viongozi wote wa Serikali, Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji tushirikiane kutokomeza dawa za kulevya”