Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama imefanya operesheni ya siku nane (8) mfululizo mkoani Morogoro katika wilaya za Morogoro, Morogoro vijijini na Mvomero na kukamata jumla ya gunia 131 za bangi kavu iliyotayari kusafirishwa, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketeza jumla ya hekari 489 ya mashamba ya bangi ambapo jumla ya watuhumiwa 18 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.
Operesheni hiyo iliyofanyika katika wilaya ya Morogoro vijijini kata ya Kisaki, kijiji cha Rumba zimekamatwa gunia 70 za bangi, Kijiji cha Mbakana zimekamatwa gunia 59 za bangi, kilo 120 za mbegu za bangi na kuteketezwa hekari 350 za mashamba ya bangi. Aidha, wilayani Mvomero Mamlaka imeteketeza hekari 139 na wilaya ya Morogoro zimekamatwa gunia mbili (2) za bangi.
Kamishna jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, wakulima wa bangi wanalima mashamba yao katika maeneo ya mbali, yaliyojificha na yasiyoweza kufikika kirahisi. Pia, wanalima pembezoni mwa mto, na kukata miti ili waweze kupata maeneo ya kulima bangi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa