‘Na Penina Malundo,TimesMajira
KAMPUNI ya Kimataifa ya Vinywaji vya Heineken, imezindua rasmi sherehe ya kimataifa ya ‘Afterwork By Heineken’ ikiwa na lengo la kuwakutanisha wafanyakazi kutoka maeneo mbalimbali kuwa pamoja.
Hayo ameyasema mwishoni mwa wiki, Meneja Mkazi wa Heineken Beverages Tanzania,Obabiyi Fagade mara baada ya kuzindua sherehe hiyo katika Mgahawa wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam
Obabiyi amesema, Afterwork By Heineken’ imeundwa kutoa mazingira ya kuvutia na ya kufurahisha kwa wafanyakazi kupumzika na kuungana pamoja baada ya siku ya kazi.Amesema, kutokana na siku ya kazi kuwa na mambo mengi hivyo Heineken imeamua kuja na sherehe hizo kwaajili ya kutoa fursa ya kuungana na wengine katika kupumzika kwa pamoja.
‘Katika jamii ya leo,kuwa na nguvu kazi yenye afya na motisha kunahusiana sana na dhana ya uwiano kati ya kazi na maisha, ambayo ni muhimu kwa kukuza nguvu kazi na taifa lenye mafanikio,”amesema na kuongeza
”Tunayo furaha kuwaletea sherehe hii ya ”Afterwork By Heineken” kwa wateja wetu wa muhimu nchini Tanzania na tumevutiwa sana na mafanikio ya tukio letu la kwanza hapa,”amesema.
Hata hivyo amesema, ‘Afterwork By Heineken’ imeundwa kuleta mazoea ya kipekee ambapo wateja wao wanaweza kufurahia kila kinywaji na kuthamini ujazo uliopo katika kila chupa.
”Idadi ya watu na hamasa tuliyoshuhudia Samaki Samaki Masaki ilikuwa ya kushangaza kwani heineken ina nuru la kuwaleta watu pamoja natunafurahi kuwa tunajenga fursa mpya za kuimarisha umoja,”amesema.’
Afterwork By Heineken’ imekuja baada ya uzinduzi wa hivi karibuni wa jalada mpya ya Heineken Beverages nchini Tanzania.
Mafanikio ya tukio hili ni hatua muhimu katika juhudi za Heineken za kuunganisha na wateja nchini Tanzania huku ikiongeza uwepo wake kimataifa na kuongeza utamaduni wa ubunifu na furaha katika masoko mapya.
Amesema, heineken ni kampuni ya kimataifa ya vinywaji ambayo ilianza tangu mwaka 1864,inafanya kazi katika zaidi ya nchi 70,ikiwa na aina mbalimbali za bia na cidar.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ