Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
MSANII wa muziki wa Bongo fleva na bosi wa Kondegangs, Rajab Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kushiriki katika uzinduzi wa album yake mpya ‘Muziki wa Mama’ iliyofanyika Mei 25, mwaka huu, kwenye ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Akitoa shukrani hizo kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, Harmonize, alisema amefarijika sana ujio wa Rais hasa kuinua sekta ya sanaa iliyoajiri vijana wengi zaidi pengine kuliko sekta nyingine yoyote.
“Tunaye Rais mwenye mapenzi makubwa na nchi yetu, Tunaye Mama msikivu aliyetenga muda wake kuja kutusikiliza na kuzifungua njia mpya ambazo hatukuwahi kuzipita.
“Binafsi nimefarijika zaidi na mpango huu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Nimefarijika pia na juhudi zake endelevu za kuyagusa makundi mbalimbali ambayo kimsingi yanamchango mkubwa kwenye uchumi wa taifa,” amesema Harmonize.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA