December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hanan’g yan’gara miradi iliyokaguliwa na Mwenge, viongozi wapongezwa

Na Mary Margwe, TimesMajira Online Hanang

Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Mwaka Kitaifa 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma  amesema Halmashauri ya wilaya ya Hanang mkoani Manyara, ni moja ya Halmashauri iliyofanya vizuri mara baada ya kuipitia miradi sita (6) yenye thamani ya sh.bil.1 na kukagua kwa kina.

Hayo aliongea juzi wakati  alipokua akizungumza na uongozi wa Halmashauri hiyo mbele ya mkuu wa wilaya hiyo  Janeth Mayanja, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Elizabeth John Lusingu akiwaaga na kuendelea na kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.

Gararuma alisema serikali imekua ikiwekeza pesa nyingi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali, isipokua katika suala la kusimamia miradi ikamilike kwa wakati na kwa ubora hilo ndio huwa ni tatizo sugu, kwani miradi mingi huwa inatekelezwa chininya kiwango na pia kusua sua katika ukamilishaji wake.

” Sisi huku hatukuja kumuonea mtu hapana, tumekuja kukagua miradi na kuangalia uhalisia wa pesa zilizotumika kama zinaendana na ubora wa mradi husika, hivyo msione kama tunawaonea wala nini mwisho wa siku wote tunafurahia uwepo wa miradi yenye viwango vilivyokidhi mahitaji yetu” aliongeza Kiongozi huyo.

Kufuatia kufanya vizuri kwa halmashauri hiyo katika miradi alimpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Elizaberth John Lusingu, Mweka hazina wa halmashauri hiyo (DT) Dunstan Nyangu, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Rose Kamili pamoja na viongozi wengine kwa ushirikiano wao na hatimaye kuweza kufanikisha kuwa na miradi yenye viwango.

Pia alisema miradi hiyo sita iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru yote  imethibitishwa na kuongeza pongezi kwa Taasisi za Ruwasa, Tarura, Halmashauri na wote waliohusika kutekeleza miradi hiyo.

Hata hivyo Kiongozi huyo wa Mwenge amewataka viongozi hao kutokubweteka na matokeo mazuri waliyoyapata na badala take waongeze juhudi katika kusimamia miradi ikamilike kwa wakati nankwa uborabunaotakiwa na si vinginevyo, huku akiwataka kuzingatia miongozo na vifungu mbaimbali vinavyoruhu matumizi ya fedha inayoruhusu kufanyika kwenye miradi husika.

Aidha alisema hakuna Maendeleo yanayofikiwa kwa kufanya man mtu mmoja, bali ushirikiano wa dhati kwa viongozi na ushirikiano na madiwani na wataalam ndio mambo yanakwenda vizuri kwa ufasaha zaidi.

” Ndugu zangu hakuna maendeleo yanayopatikana kwa haraka kwa kufanmywa na mtu mmoja peke yake , tunapokaa pamoja na kila mmoja akaitoa kikamilifu katika uwajibikaji wake ndio tunapata ushirikiano mkubwa mahala pa kazi, hivyo nawapongeza viongozi wote niliowataja na nisiowataja kwani miradi tumeipitia na kuikagua iko katika viwango tunavyotaka” alisema Geraruma.

Aidha aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanafanya marekebisho pale waliposhauri wahakikishe wanarekebisha zile dosari ndogo alizowaachia kufanyiwa marekebisho ili miradi iweze kuleta tija katika jamii na hatimaye kuendelea kuwa na mazoea na kumiliki vitu vilivyo na ubora ukilinganisha na miaka ya nyuma miradi mingi ilikua ikigharimu fedha nyingi huku haiwi na ubora unaohotajika.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Janeth Mayanja alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika halmashauri ya wilaya ya Hanang imetembelea miradi 6 Kati ya hiyo miradi miwili ilizinduliwa, mradi mmoja uliwekewa jiwe na Msingi, miradi mitatu ilionwa.

Mayanja alisema Mwenge huo umewasaidia kuwa chachu kubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii, ambapo miradi hiyo 6 ni ya thamani ya sh.bil.1.

” Kati ya Miradi sita, Mradi wa Maji Gidangu – Gidahababieg wenye thamani ya sh.mil. 120, Mradi wa ujenzi wa madarasa manne Nangwa Sekondari kwa thamani ya shmil. 84, Mradi wa ujenzi wa jengo la dharura Hospitali ya Tumaini wenye thamani ya sh.mil. 300″ alisema mkuu huyo wa Wilaya.

“‘Miradi mingine ninujenzi wa madarasa mawili Ganana Sekondari  wenye thamani ya sh .mil.38 Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami barabara ya Mkapa wenye thamani ya sh .mil. 499 na mradi wa kikundi cha vijana  Dream Studio and Stationery wenye thamani ya sh.mil. 15 Kata ya Katesh” alifafanua Mayanja.

Miradi hiyo sita iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru yote  imethibitishwa na kutoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang Bi Janeth Mayanja Taasisi za Ruwasa, Tarura, Halmashauri na wote waliohusika kutekeleza miradi hiyo.

Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru amehimiza Watumishi kusimamia miradi kwa wakati na kuzingatia miongozo.