December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Hamisa Mobetto ateuliwa kuwa Balozi Spaghetti

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

MWANAMITINDO Hamisa Mobeto, ametambulishwa kuwa Balozi wa bidhaa ya tambi aina ya Spaghetti inayotengenzwa na kampuni ya Azania Group.

Mobeto ametambulishwa leo, Julai 26, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Joel Laizer na kufafanua kuwa bidhaa hiyo ina miezi sita tangu kuingizwa sokoni. 

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Mobeto alisema kuwa alikuwa akiitumia bidhaa hiyo Kwa kipindi kirefu na ni furaha kwake kuwa Balozi na anaamini atafanya vema kuhamasisha jamii kuzitumia. 

“Naamini watanzania wataitumia kutokana a na ubora wa bidhaa tofauti na nyingine, hivyo nawaomba jamii kubwa wajitokeze kuitumia,”amesema Laizer

Awali Mkurugenzi, Laizer, alisema kuwa bidhaa hiyo inautofauti mkubwa na nyingine hivyo ni huu ndio wakati sahihi kuitumia.

Hii bidhaa inaradha nzuri na haikamatiki kama nyingine hivyo ubora wake ni mkubwa tofauti na nyingine,”amesema