November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Halmashauri zatakiwa kutenga pesa za mikopo kwa vikundi vya waviu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga amepongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka 3.5% mwaka 2020 hadi kufikia 3.2% kwa mwaka 2021.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti Mpya ya serikali 2022-2023 itakayoanza mwezi wa saba ameongeza fedha eneo kutoka Billion 1 Mpaka Billion 1.8”

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa wa Tanga ya Mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi.

Aidha Naibu Waziri Mhe. Ummy Nderiananga ameshauri Halmashauri za wilaya kuona umuhimu wa kutenga fedha za Mapambano Dhidi ya Virusi vya Ukimwi. Hii itasaidia kuwawezesha katika miradi ya vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (WAVIU) kufanya shughuli zao za maendeleo vizuri.

Wananchi msiogobe kujitokeza kupima virusi vya ukimwi, mpime mjitambue afya zenu. Kama Kauli mbiu inavyosema pima VVU, Jitambue ishi alisema Naibu Waziri Ummy

“Mabinti mnao toa elimu rika, endeeleni kuwaelimisha mabinti wenzetu. Asilimia kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi yapo kwa vijana na asilimia 80% ya hao vijana ni mabinti lazima tuendele kuelimishana, Naibu waziri Ummy”

Naye Naibu katibu Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya amesema Baraza la Watu Waoishi na Virusi Vya Ukimwi ambao wamejitokeza na kujitangaza na kusema wako tayari kushirikiana na serikali kutoa elimu (NACOPHA) ni baraza muhimu.

“Hili baraza ni rasilimali kubwa sana kufikia malengo yetu, wanaishi kwa mfano na wanamalengo na wanatusaidia hata wale walioachaa dawa kwa sababu mbalimbali wanawatafuta na kuongea nao na kuwarudisha kwenye dawa alisema, Naibu Katibu Mmuya”

Ninaomba hizi afua mbalimbali za ukimwi zinazofanyika, maelekezo yatoke mradi wowote unahusu mambo ya ukimwi washirikiane na NACOPHA. Hawa wanauwezo wa kufikia walengwa mpaka ndani kijijini na wanatusaidia kufikia malengo ya taifa kwa kutumia muda vizuri na fedha vizuri.

Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Tanga alipokuwa akipokea taarifa ya Mkoa huo ya Mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi.
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akiwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmuya alipotembelea shule ya Msingi Majani Mapana na shule ya Sekondari Nguvu Mali kujionea utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Bi. Bahati Mohamedi Katibu wa Konga jiji la Tanga alipotembelea katika ziara yake kujionea shughuli za kiuchumi za WAVIU.
Naibu Waziri Ofisi yaWaziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akimsikiliza Bi, Halima Ally Mbabe Muelimisha rika alipokuwa akieleza shughuli wanazofanya katika Konga ya Jiji la Tanga.