Na Esther Macha ,TimesMajira,Online,Mbeya
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya limepata viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika Jana mjini Lujewa.
Katika uchaguzi huo, Twalib Lubandamo amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri hiyo ambayo kwa miaka mitano iliyopita iliongozwa na Francis Mtega ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mbarali.
Lubandamo ambaye alikuwa Mgombea pekee wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), alichaguliwa kwa kura 26 za ndiyo huku kura moja ikimkataa kwa kupigiwa kura ya hapana.
Kwa Upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wa hiyo ilinyakuliwa na Mbwanjine Jeremiah aliyepata kura 26 za ndiyo
Akitangaza matokeo hayo, Kaimu Afisa Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Oliva Sulle amesema hakuna kura iliyoharibika na kwa mamlaka aliyonayo akawatangaza rasmi washindi wa uchaguzi huo kuwa viongozi wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Aidha Sulle amewataka madiwani wote kwa pamoja kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa ili waweze kushirikiana nao katika kuleta maendeleo kwenye kata zao.
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024