Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
HALMASHAURI KUU ya CCM kata ya Msongola wafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo ya Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan ,ndani ya kata ya Msongola.
Ziara hiyo imeandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Azizi Mwalile , katika kuangalia utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi yale aliyoyafanya katika uongozi wake ambapo Diwani Azizi Mwalile wajumbe wa Halmashauri Kuu walitembelea miradi ya Serikali sekta ya Elimu ,sekta ya afya na kuangalia miundombinu ya Barabara.
Akiongoza ziara hiyo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Msongola MAHANDO MWITA, alipongeza utekelezaji wa Ilani ya chama miradi mikubwa ya maendeleo ambayo imetekelezwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano wasimamizi wake Mbunge wa Ukonga Jery Silaa na Diwani wa Kata hiyo Azizi Mwalile.
“HALMASHAURI kuu mimi na Wajumbe wangu tumelizishwa na utekelezaji wa Ilani sekta ya afya upanuzi wa vituo vya afya Mvuti , sekta ya Elimu shule za Kisasa zimejengwa kata Msongola ” alisema Mahando.
Mwenyekiti Mahando alisema Diwani wa Kata ya Msongola anatarajia kuwasilisha Ilani ya chama kabla kuwasilisha ILANI Wajumbe wa Halmashauri Kuu lazima wafanye ziara kukagua miradi ya maendeleo na leo Wajumbe wote tumelizishwa na Utekelezaji wa Ilani.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti Mahando aliwataka Walimu Wakuu wote katika shule za Serikali kusimamia miradi ya maendeleo vizuri ambayo imeelekezwa katika kata hiyo na ijengwe kwa viwango kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Serikali za mitaa ili kama kuna changamoto waweze kuzichukua kuwasilisha ngazi ya juu .
Aidha aliwataka Wakuu wa shule na Walimu wa Shule za Msingi kufanya kazi kwa weledi ikiwemo kuongeza Taaluma shuleni ili wanafunzi waweze kufaulu kwa kiwango cha juu.
Diwani wa Kata ya Msongola AZIZI MWALILE aliwashukuru Wajumbe wa Halmashauri kuu kwa kutembelea Miradi ya maendeleo inayotekekezwa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu ambapo aliwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu walitembelea miradi mikubwa ya Serikali washirikiane pamoja katika kuitunza na kukisemea chama vizuri.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa kwa ushirikiano wake katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Ukonga hususani kata ya Msongola maendeleo yake kwa sasa yanakuja kwa kasi.
Katika ziara hiyo Wajumbe wa Halmashauri walitembelea Mondole,kuangalia matundu kumi ya vyoo,shule ya Msingi Kitonga ambapo zimetolewa shilingi milioni 60 Madarasa na vyoo na ujenzi wa Madarasa mapya unaendelea ujenzi ulianza April na Juni utamalizika ,Mtaa wa Mivuleni Jengo la Utawala ,vyoo vya madarasa wametenga milioni 150 ambapo kwa sasa wapo katika hatua ya kufunga linta MVUTI ujenzi wa kituo cha afya cha kisasa,shule ya msingi Kiboga,Shule ya Sekondari Sabodo.
Kwa Upande wake Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala MAGDALENA THOMAS alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge Jerry Silaa na DiwaniMwalile, kwa kuwekeza sekta ya elimu na Afya kata ya Msongola yenye shule nyingi za Serikali za msingi na Sekondari.
Diwani Magdalena aliwataka Wajumbe wa Halmashauri Kuu kuilinda miradi ya Serikali ikiwemo kufanya ziara kukagua kila wakati kuangalia utekelezaji wa Ilani waweze kwenda kuwaeleza wananchi juhudi za Serikali.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi