Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline,Dar es Salaam
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam, imetangaza kuanza rasmi kukusanya kanzi data kwa wafanyabiashara wote Jijini humo, lengo likiwa kuboresha huduma za kibiashara.
Hayo yamesemwa,Jijini Dar es Salaam leo,Agosti 15,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo wakati akizungumzana na waandishi wa habari,hatua imekuta kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akizindua Mkongo wa Taiafa hivi karibuni,kuwataka wafanyabiashara wote kuingia katika mfumo ili kuzuia wanaokwepa kulipa kodi.
Mpogole amesema kuwa licha ya kuwabaini walipa kodi lakini pia wafanyabiashara hao wakiingizwa kwenye kanzi data itakuwa rahisi kuwafikia kwa urahisi zaidi.
“Hadi sasa tayari vimeanzishwa vituo saba ambavyo vitatumika kutoa huduma kwa wafanyabiashara ili kutopata changamoto ya upatikanaji wa huduma za kibiashara kama upatikanaji wa leseni na ulipaji wa ushuru,”amesema Mpogole.
Aidha amesema kuwa vituo hivyo pia vitaweza kutumiwa na Mamlaka za mapato TRA, katika ufanyaji wao wa kazi pindi wanapotaka kuwafikia wafanyabiashara,ambapo amesema zoezi hilo linatarajiwa kuanza Septemba 1 hadi 14 mwaka huu.
Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa ufanyikaji wa zoezi hilo na kuwataka kufika Ofisi za Serikali za Mitaa pindi wanapokuwa na hofu juu ya ujio huo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa