Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
SERIKALI ya jamhuri ya muungano wa Tanzania itashirikiana na chama cha watu wenye ualbino kuhakikisha mapitio ya sera na haki za watu wenye ualbino zinatekelezwa kwa umakini mkubwa.
Akizungumza Mkoani pwani katika maadhimisho ya 19 mgeni rasmi mkuu wa mkoa huo Abubakari Kunenge aliyemuwakilisha waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu amesema watu wenye ualbino ni jamii yetu hivyo Wana haki na wajibu wa kuishi katika Taifa hili.
“Serikali itaendelea kuyapa kipaumbele masuala yote yanayofanywa na watu wenye ualbino kwa kutambua kuwa wana haki ya msingi kuishi bila kubaguliwa na mtu yeyote,”amesema Kunenge
Aidha serikali iko makini katika kufuatilia mapitio ya sera mbalimbali na kukomesha vitendo hatarishi vinavyo hatarisha amani dhidi ya jamii ya watu wenye ualbino.
Hata hivyo watu hawa watashirikishwa katika mipango mbalimbali ya kimaendeleo kiuchumi iwe kuchugua ama kuchaguliwa katika chaguzi zilizo mbeleni mwetu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TAS Taifa Godson Mollel amesema Sheria za nchi zichukue nafasi kuwachukulia hatua walioshiriki utekaji wa tukio lililotokea Muleba kwa kumteka mtoto mwenye ualbino mwenye umri wa miaka 2 na nusu.
Ameendelea kusema wanamuomba rais dokta Samia Suluhu aweze kukutana na chama cha watu wenye ualbino kwa ajili ya kuzungumza nae masuala mbalimbali.
Mwenyekiti huyo amewataka watu wenye ualbino kuwa watulivu huku taratibu na hatua stahiki dhidi ya ulinzi wao ukichukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama na raia wema.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano