Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha
Waziri wa jinsia,wanawake,na makundi maaalumu Dkt Dorothy Gwajima amewataka wadau wa maendeleo nchini kuhakikisha kuwa wanajifunza sekta ya maendeleo pamoja na programu mbalimbali kutoka katika taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru Ambapo kwa sasa wameweza kufanya programu mbalimbali ambazo ikiwemo ya Mafunzo ya Elimu ya fedha ambayo Kwa sasa ni programu ambayo inahitajika sana ndani ya jamii.
Dkt Gwajima ameyasema hayo wiki iliyopita wakati akifungua rasmi Mafunzo ya sekta ya fedha ambayo yaliwashiriisha vijana 100 kutoka taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru Ambao sasa watakuwa mabalozi katika sekta ya fedha lakini pia maendeleo ya Jamii.
Dkt Gwajima amesema kuwa taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru imekuwa ni moja ya taasisi ambayo inabuni njia na mikakati mbalimbali ya kijamii na hivyo hata wahitimu wake wanakuwa mabalozi wazuri hasa kwenye sekta ya Jamii
“Nikiwa kama waziri mwenye dhamana nataka niwapongeze hasa kwa programu hii ambayo mmeweza kuibuni na sasa niseme kuwa sekta ya fedha ni moja ya nguzo ambayo inaenda sambamba na maendeleo ya Jamii”amesema Dkt Gwajima
Katika hatua nyingine amesema kuw Sekta ya fedha bado inakabiliwa na changamoto ya uelewa mdogo sana na ili changamoto hiyo inatakiwa iweze kutatuliwa na maafisa maendeleo ya Jamii
Amesisitiza kuwa kwa sasa maafisa maendeleo ya Jamii pamoja na wanafunzi katika sekta hiyo wanajukumu jukumu kubwa sana la kuhakikisha kuwa wanasema sekta ya fedha ikiwa ni pamoja na kuwaonesha Wana jamii fursa zilizipo kama zinazoorodheshwa
“Bado jamii haina uelewa wa kutosha juu ya elimu ya fedha lakini hata fursa hazijukikani inatakiwa afisa maendeleo nao wawe chachu ya kuleta ajira kwa kuwaelewesha wananchi juu ya fursa ambazo zipo ili kupunguza Kasi ya umaskini”ameongeza
Pia alisema Kwa kutambua kuwa umuhimu wa programu hiyo bado Serikali itaendelea kuwashika mkono Taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru ili waweze kuboresha programu ya hiyo ambayo Kwa sasa inaitajika sana.
Naye mkuu wa taasisi hiyo ya maendeleo ya Jamii Tengeru,Dkt Bakari George amesema kuwa taasisi kwa kutambua umuhimu wa maendeleo ya Jamii pamoja na fedha wamekuwa wakishirikiana katika sekta ya fedha ili kupunguza umaskiniBakari alisema kuwa taasisi pia imeweza kuingia kwenye makubaliano na taasisi mbalimbali ambazo zinatoa elimu hasa ya fedha ambapo washiriki ambao wameshiriki wameweza nao kuunda vikundi ambavyo vimepata usajili.
Amehitimisha kwa kusema Kuwa taasisi ya maendeleo ya Jamii Tengeru Sasa inapanga kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kutoa Elimu ya fedha Kwa wakufunzi,wanafunzi ili waweze kuielezea sekta ya fedha ambayo inaenda sambasamba na maendeleo ya Jamii.
More Stories
‘Ni Wasira ‘Makamu Mwenyekiti CCM Bara
15 mbaroni tuhuma wizi wa shehena ya unga wa sembe
Wacheza rafu Uchaguzi Mkuu ujao waonywa