Na Penina Malundo, timesmajira
NCHI za Tanzania, Burundi na Rwanda zimeunganishwa kikamilifu kwenye gridi za umeme kupitia Mradi wa Umeme wa Maji wa Maporomoko ya Rusumo wa Megawati 80.
Hayo yalisemwa hivi karibu na Meneja Mradi wa Rusumo, Mhandisi Aloyce Oduor wakati akiongea na waandishi wa habari,amesema Februari 2024,mchakato wa kuunganisha Gridi za Umeme za Tanzania, Burundi, Rwanda ulikamilika kupitia Mradi wa Umeme wa Rusumo Falls wa Mkoa wa 80MW.
Amesema unganishaji na usawazishaji wa gridi ya umeme kati ya nchi hizo tatu umekamilika kupitia bwawa la pamoja na kuzipa fursa nchi hizo kufanya biashara ya umeme.
“Uunganishaji wa gridi kati ya Tanzania ,Burundi na Rwanda umekamilika kikamilifu na kutengeneza njia ya pamoja ya upatikanaji wa umeme na hii kuruhusu uuzianaji wa nishati baina ya nchi hizi tatu ,’ amesema Oduor.
Amesema mtandao wa usafirishaji wa umeme kati ya Rwanda, Burundi na Tanzania (Rusumo network) una urefu wa kilomita 372 za usafirishaji wa umeme mkubwa(OHTL) wa kV 220.
“Laini za usafirishaji umeme kwa nchi ya Burundi zinaanzia Rusumo hadi Muyinga na kuendelea hadi Gitega, OHTL ya kilomita 160,”alisema na kuendelea;
“Kwa nchi ya Rwanda, laini ya usafirishaji wa umeme mkubwa (OHTL) inaanzia Rusumo hadi Bugesera na kuendelea hadi Shango,yenye urefu wa kilomita 118,wakati ya Tanzania inaanzia Rusumo hadi Nyakanazi ambayo ni kilomita 94.”amesema.
Amesema laini zote za usafirishaji umeme na vituo vya kupoozea umeme vimekamilika na vipo kwenye majaribio tangu Novemba 3, 2023 hadi Januari 31, 2024,ambapo jumla ya nishati inayozalishwa ni KWh milioni 66 ambayo ilisafirishwa na kupelekwa katika laini za kusafirishia umeme za nchi hizo.
“Ukikamilika, muunganiko huu utazipa fursa nchi hizo za kufanya biashara ya nishati kati yao na hata kwa nchi jirani kupitia makubaliano ya uuzianaji “wheeling” ya umeme,”amesema Ofisa Mipango wa Kanda wa NELSAP-CU wa Nishati na Biashara Mhandisi Jacob Manyuon Deng.
Mhandisi Deng amesema ushirikiano huo ulifadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika(AFDB) kwa kiasi cha dola za kimarekani 120 na utakapokamilika utaweza kutoa fursa nchi hizo za kufanya biashara ya nishati kati yao na hata kwa nchi jirani kupitia makubaliano ya uuzianaji wa umeme,”amesema.
Amesema mradi huo ukikamilika kupitia muunganiko huu utazipa fursa nchi hizo kufanya biashara ya nishati kati yao na hata kwa nchi jirani kupitia makubaliano ya uuzianaji
Mhandisi Deng amesema makubaliano hayo yanaruhusu nchi mbili ambazo hazipakani kuuziana nishati kupitia mtandao wa nchi ya tatu kwa ada.
”Mashirika ya nishati ya Umeme ya nchi hizo tatu zinazosimamia njia za usafirishaji umeme ikiwemo, Shirika la Umeme wa Umeme Tanzania (TANESCO),Shirika la Usambazaji Umeme la Burundi( Régie de Distribution(REGIDESO) na Shirika laNishati la Rwanda Energy Group (REG-EUCL) zilitia saini ya mkataba wa manunuzi ya Umeme (PPA)na RPCL kwa tarehe tofauti,amesema na kuongeza
”Shirika la REGIDESO ilitia saini PPA Juni 21, 2023, TANESCO ilitia saini Septemba 30, 2023, wakati REG-EUCL ilitia saini Desemba 1,2023,”amesema.
Amesema mkataba wa ununuzi wa Umeme (PPA) ni makubaliano ya kimkataba kati ya wanunuzi na wauzaji wa nishati hivyo kwa pamoja walikubaliana namna watakavyonunua na kuuza nishati inayotokana na mradi.’Chukua au Lipa Modeli’
Mhandisi Deng amesema mkataba wa ununuzi wa umeme uliotiwa saini kwenye Mradi wa Rusumo na mashirika ya usambazaji ya nishati hiyo kwa nchi hizo tatu utafanyika kwa mtindo wa ‘chukua au lipa.’
Amesema nchi ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ziliunganisha gridi zao miaka sita iliyopita kupitia njia ya kusafirisha umeme ya Rubavu-Goma,hivyo kupitia mradi huu kama Tanzania na Rwanda zinaweza kukubaliana juu ya makubaliano ya “wheeling’’.
Mhandisi Deng amesema Tanzania inaweza kuja kuuza umeme wake wa ziada kutoka kwenye miradi ya umeme ijayo kwa nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.
More Stories
The Desk & Chair yashusha neema Gereza la Butimba
TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo
TAKUKURU,yasaidia kurejesha hekali 8