Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe mapema leo amemkabidhi ofisi Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni Saadi Mtambule katika kuhakikisha anaendelea kumuwakilisha vyema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa shughuli zote za serikali.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo jijini Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuamini kuwa tunauwezo wa kumsaidia haswa katika ngazi ya wilaya ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo, amani na uchumi wao kukua.
“Ukizungumzia mapato ya ndani katika mikoa 33 ya Tanzania Nzima, tunachangia asilimia 20 ya mapato nchini na kwa upande wa kinondoni tumekuwa tukikuwa kila wakati kuanzia bilioni 49 msimu uliyopita, kwa sasa bilioni 57.2 na sasa utakwenda mpaka bilioni 61 yoteb hayo nikuhakikisha mapato yanakuwa” amesema Gondwe
“Naomba mnipe ushirikiano wenu kama mlivyompa Mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Godwin Gondwe, mnipe kwa pande zote mbili ili kuhakikisha tunasimamia taasisi zetu kwa mujibu wa sheria na taratibu bila kuiingilia halmashauri yetu na kufanya kazi zake pasipo na kikwazo” amesema Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saadi Mtambule
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa