November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

GF  Trucks  yachukua ushindi wa jumla katika sekta ya Magari na mitambo  sabasaba   

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wakati maonyesho ya biashara ya ya kimataifa yakihitimishwa rasmi  zaidi ya makampuni 300 ya ndani na nje ya nchi yameshiriki maonyesho hayo huku nchi 26 zikiwa zimeshiriki maonyesho hayo yaliofunguliwa tarehe 03 mwezi julai na Rais Samia Suluhu Hassani  na kufungwa na Rais wa Zazibar, Dk Hussen Ali Mwinyi.

Kabla ya kuhitimishwa kwa maonyesho hayo kulitanguliwa na kutembelea mabanda mbali mbali na miongoni mwa banda lililotembelewa ni la kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd.

Akiwa bandani hapo aliweza kujionea magari mbalimbali yanayotengenezwa nchini na kampuni hiyo yenye kiwanda chake kilichopo Kibaha mkoani Pwani miongoni mwa magari hayo ni FAW,Hong yan,Forland pamoja na mitambo ya xcmg.

Akizungumza wakati  Rais akiwa katika banda la kampuni hiyo ya GF  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa GF group ,Mahboob Karmal alisema ombi  lao kwa serikali ni kuona ni jinsi gani wanaweza wakarekebisha sheria za uagizaji wa magari yaliotumika(used) ili kulinda viwanda vyetu na kwani GF wao wanauwezo wa kuunganisha magari madogo lakini ukiangalia ushindani tulionao na magari yaliotumika (used car)ni mkubwa.

Kampuni hiyo pia imeibuka mshindi wa jumla katika kipengere cha uunganishaji wa magari na Uuzaji wa mitambo pamoja na mashine za ujenzi katika kampuni yao ya uzaji wa magari  ya GF Automobile  wameibuka washindi katika kipengere cha Usafirishaji .

Pia tuzo ya pili ni katika sekta ya Mitambo na mashine  na Teknolojia wamekuwa  washindi wa jumla katika maonyesho hayo.

Kufuatia hilo Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Alli Mwinyi ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) kuendelea kufanya utafiti wa masoko yanayopatikana ndani ya bara la Afrika na kutoa taarifa kwa wafanyabiashara.

Dk Mwinyi amesema matokeo yaliyopatikana kupitia maonyesho haya yameonyesha namna fursa ya kukuza bishara ilivyotumiwa vizuri na kampuni za ndani huku akieleza kuwa matokeo zaidi yataonekana kupitia kushamiri kwa biashara, kukuza ajira na na kulinda viwanda vya ndani.
 
“Hivyo ninaziagiza wizara zote zenye majukumu ya kusimamia biashara nchini washirikina kutatua changamoto zote zinazojitokeza,” amesema Dk Mwinyi.
 
Dk Mwinyi amesema kama nchi inayo fursa ya zaidi ya soko katika Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA), soko la Afrika ya Mashariki (EA) na Soko la nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (Sadc).
Amesema miongoni mwa bidhaa zenye soko ndani na nje ya nchi ni Samaki, dagaa, mwani, sukari, mafuta ya kula huku akitaka uzalishaji ufanyike kwa ajili wa kutosha na ziada.
“Na nimeelezwa kuwa kuna masoko tisa ya nje yamepatikana ikiwemo Afrika Kusini, Malawi, Uturuki, Saudi Arabia hivyo muongeze bidii ili tufikie masoko haya,” amesema Dk Mwinyi.
 “Pia tathmini inaonyesha maonyesho yamewapa fursa ya kupata wabia wa biashara na kutengeneza uhusiano mzuri hivyo  wizara ya Viwanda na bishara kwa kushirikiana na Tantrade saidieni kuondoa vikwazo visivyokuwa vya kikodi,” amesema Dk Mwinyi.
Pia alitaka kuondolewa kwa urasimu ili kuwezesha biashara zaidi huku akisema serikali itaendelea kuhamasisha uwezekezaji hasa katika maeneo ya kimkakati huku ikiondoa kodi na tozo, ikiweka mazingira mazuri ya biashara na kufanya mifumo isomane.
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx