January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

GF Trucks & Equipment yadhamini uzinduzi wa Umoja wa Wamiliki wa Magari Makubwa na Mitambo (Mashine).

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online

KAMPUNI ya GF Trucks & Equipment yadhamini uzinduzi wa umoja wa wamiliki wa magari makubwa na mitambo (Mashine) kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuwawezesha watanzania kupata ajira ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya GF Trucks na Equipment, Smart Deus amesema kuwa kampuni hiyo iliamua kudhamini Chama hicho ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha watanzania kupata ajira.

“Tumeona kuwa wengi wa wateja wetu ni wanachama wa chama hichi kwa hiyo ikatusukuma kudhamini  chama hichi kwa lengo la kukuza ajira, pili wateja wetu na kuhamisisha na kuunga mkono juhudi za  Viwanda Tanzania.

Aidha, hiyo ikiwa ni sehemu ya GF Trucks & Equipment kusherekea miaka 15 katika Biashara.