Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Kampuni ya GF Trucks & Equipment na EFTA ya mikopo imeingia makubaliano ya kuwakopesha wakulima na wafugaji vifaa mbalimbali vya kilimo na vitendea kazi muhimu kuelekea maonesho ya nanenane mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko kutoka GF Trucks, Bw Salman Karmali alisema kwamba makubaliano hayo ya kibiashara ya nia ya kuwawezesha wakulima na wafugaji hapa nchini.
“sisi ni wauzaji wa magari makubwa na mitambo pia ni wauzaji wa vipuri vya magari na tunatoa huduma ya matengenezo makubaliano haya yanafungulia milango kwa wakulima na wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa mazao kuweza kusafirisha bidhaa zao kwa haraka na kufikia masoko,” alisema Bw Karmali
Aliongeza kwamba kupitia makubaliano hayo ya kibiashara wakulima, wafugaji na wafanyabiashara watapata fursa ya kutembelea banda la GF Trucks na EFTA ambapo watakuwa pamoja na kuweza kuwapa taarifa mbalimbali juu ya mikopo ya magari na vifaa vya kilimo kama vile Trekta na power tiller.
Alifafanua kwamba wateja wa GF Trucks wanaweza kupata huduma za kifedha kupitia EFTA ambao ni wadau wao wakubwa kwenye kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa watanzania wengi.
Alisema kwamba wateja wa kampuni hiyo wanaweza kufanya malipo ya awali kwa asilimia 20 na kupata gari au kifaa cha kilimo ndani ya siku 5 na kupewa muda wa malipo ndani ya miezi miwili.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya EFTA , Bw Clerius Asiel alisema kwamba kampuni hiyo imefanya kazi hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 ina uzoefu kwenye huduma za mikopo na fedha.
“hii ni kampeni kabambe kwa wakulima na wafugaji kuelekea kwenye nanenane wataweza kupata mikopo ya magari , matreta na vifaa vingine vya kilimo ili kuweza kuinua na kukuza kilimo hapa nchini.
Bw Asiel aliongeza kwamba kwa kipindi chote walichokaa hapa nchini wameweza kutoa mikopo dola za kimarekani 100 milioni (Tsh bilioni 300) kwa watanzania mbalimbali.
Alisema kwamba pamoja na mambo mengine kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini Dr Samia Suluhu Hassan za kuendeleza kilimo na kukuza mnyororo wa thamani.
Alisema kwamba katika kipindi cha nanenane kampuni hiyo mbili zitakuwa kwenye mikoa ya Arusha, Dodoma, Mbeya , Mwanza na Morogoro ili kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji na wafanyabiashara kuchangamkia fursa hizo za mikopo yenye riba nafuu.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba