Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
Mamlaka ya Maji na Usafi na Mazingira mjini Geita yabainisha mikakati ya kumaliza na mipango ya kuhakikisha miradi inayoendelea kutekelezwa na kukamilika kwa wakati ili kupunguza Changamoto ya upatikanaji wa Maji kwa wananchi wa Mjini.
Akizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu wakati alipotembelea banda la Geuwasa katika maonyesho ya madini yanayoendelea Mkoani Geita, Meneja wa Geuwasa Mhandisi Frank Changawa amesema Maji yanatoka kwa mgao lakini miradi mingi inatekelezwa ukiwemo ule wa miji 28 ambao unatarajiwa kukamilika oktoba 2025 ambao utaondoka kabisa tatizo la Maji.
Amesema kwa Sasa Mji wa Geita unahitaji Maji Lita Milioni 20 kwa siku pindi mradi wa chujio la nyakanga utakapokamika mwishoni mwa mwezi oktoba utasogeza mbele upatikanaji wa Maji kutoka Lita Milioni 4 inayopatikana kwa sasa mpaka Lita Milioni 7 kwa siku.
Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu ameitaka mamlaka hiyo kumalizia miradi hiyo kwa wakati Ili kutimiza adhma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani ya kumtua mama ndoo kichwani
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa