December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Gertrude Mongella asema ni Samia tu

*Asisitiza miaka yote alitamani mwanamke awe juu, asema hawezi kumtakia mabaya, afafanua hayo ni matunda ya harakati za miaka 40

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MWANASIASA mkongwe na mpigania harakati za usawa kwa wanawake nchini na duania kwa ujumla, Balozi Gertrude Mongela, amesema kushinda kwa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kinyang’anyiro cha urais itakuwa ni kushinda kwake, hivyo hawezi kumtakia mabaya akiwa juu.

“Kushinda kwake yeye (Samia), ndiyo kushida kwangu. Kila siku  nawaza, hivi Samia (Rais Samia Suluhu Hassan) akishindwa na mimi sintakuwa nimeshindwa?

Yaani mimi nilikuwa nikitamani mwanamke ashike atamu, sasa mwanamke yupo juu, nimtakie mabaya? akishindwa na mimi nimeshindwa,” alisema Mongella.

Mongella alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kutunukiwa Tuzo ya Heshima iliyoandaliwa na Clouds Media Group, huku akisisitiza kwamba;

“Nilitaka mwanamke awe juu, asiambiwe fuata ya juu, sasa mwanamke yupo hapo juu nimtakie mabaya? Akishindwa na mimi nimeshindwa,” alisema Mongella.

Aidha, Rais Samia wakati akihojiwa na Televisheni ya Taifa (TBC), Mongella, alionesha kutamani fomo moja urais 2025.  

Aliweka wazi kufurahishwa kwake kwa kuona kile walichokipigania kinapatikana baada ya miaka 40.



Mongella, kwa kipindi cha miaka 40 alikuwa kwenye harakati za kupigania usawa wa kijinsia ambazo kwa Tanzania zimezaa matunda baada ya muda huo, tangu alipoanza harakati hizo.

Aidha, Mongella alikuwa miongoni mwa wanawake waliohudhuria na kupitisha Azimio la Beijing ambalo lilifungua zama mpya ya kusaka usawa wa kijinsia, matunda ambayo yanaonekana Tanzania.

Mwaka 1995, mjini Beijing walikuwepo wanawake 12 wakuu wa nchi na Serikali, lakini hii kuna wanawake 22 wakuu wa nchi na Serikali katika Mataifa 193.”