January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Geraruma aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, kusimamia miradi yenye viwango

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Kiteto

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Sahili Geraruma ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa uwajibikaji wake katika kusimamia kujengwa miradi yenye viwango, ambapo jumla ya miradi 5 yenye thaman ya sh.bil.1.8 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru imepita yote.

Hayo alibainisha wakati akizungumza wakati alipokua akiitembelea miradi hiyo na kujionea hali halisi ya namna ya ujenzi wa miradi hiyo ilivyojenga, fedha za serikali, wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo zimekwenda kihalali Kiteto, hivyo hongereni sana kite to umeupiga mwingine hadi mmepitiliza.

Kufuatia hilo Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Geraruma alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo John Nchimbi kwa uwajibikaji wake akishirikiana na wataalam wake, huku pia akimpongeza mkuu wa wilaya hiyo Mbaraka Batenga kwa usimamizi wa miradi hiyo pamoja na madiwani.

” Mkurugenzi Mtendaji nikupongeze sana kwa juhudi kubwa unazoendelea nazo katika kuhakikisha miradi yote tuliyoipitia imesimama kikamilifu, Yaani kiufupi Kiteto mmeupiga mwingi hadi mmepitiliza, mkuu wa wilaya hongereni sana endeleeni kushikamana kikamilifu ili kuweza kufikia malengo mliyojiwekea, miradi tumeipitia yote na imekidhi vigezo, japo kuna vidosari ndogo ndogo naomba mvifanyie kazi ” alisema Geraruma.

Aidha alisema  miradi inapokua inajengwa kwa viwango hivyo inawatia moyo hata waliotoa pesa wanapata nia ya kuendelea kuchangia miradi mwingine mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika maeneo mbalimbali, hivyo endeleeni na juhudi hizo.

Aidha kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya hiyo Mbaraka Batenga alisema
Mwenge wa Uhuru ulitembelea, jumla ya miradi ipatayo 5 yenye thamani ya s. Bil.1.8.

Batenga alisema miradi hiyo ilzindua na kuweka jiwe la Msingi katika miradi mitano (5) ya maendeleo ambayo yamejengwa katika kipindi cha mwaka mmoja 2021/2022.

“‘Ujenzi wa Kituo cha Afya Tarafa ya Olboloti – Kijiji cha Mwanya kata ya Njoro  umegharimu sh.500,000,000, ujenzi  wa Shule Mpya ya Sekondari  Engusero Kata ya Namelock umegharimu sh.mil.. 600, ujenzi Mradi Maji Kaloleni kata ya Kaloleni umegharimu sh. Mil.400” alisema Batenga

Mbali na miradi hiyo aliitaja miradi mwingine kuwa ni Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Njia Panda Kata ya Namelock 50,000,000 Tshs pesa za ziada pamoja na Ujenzi wa Mradi wa Hotel ya Kilimanjaro ya Puliza mradi wa mtu  Binafsi uliogharimu jumla ya sh.mil.250.